Thursday, February 20, 2014

PPF YAANDIKISHA WANACHAMA WAPYA KATIKA TAMASHA LA MWANAMKE NA AKIBA LINALOENDELEA KUFANYIKA KATIKA UKUMBI WA DAR LIVE

Meneja mahusiano na Masoko wa mfuko wa pensheni wa PPF Bi Lulu Mengele akitoa hotuba fupi kwa washiriki waliohudhuria tamasha la wanawake na akiba ambapo PPF ilishiriki ili kuweza kutoa elimu kwa Washiriki kuweza kujua umuhimu wa kuchangia na mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mfumo wao wa hiyari katika tamasha la wanawake na akiba linaloendelea kufanyika katika Ukumbi wa Dar Live.
Mama Asha Bilali akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF mara baada ya kujiunga na mfuko wa pensheni wa PPF wakati alipotembelea banda la PPF kwenye tamasha la Wanawake na Akiba linaloendelea kufanyika katika Ukumbi wa Dar Live jijini Dar Es Salaam.
Mama Asha Bilali akimkabidhi Cheti Cha Udhamini kwa Meneja Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF katika tamasha la wanawake na akiba linaloendelea kufanyika Katika ukumbi wa Dar Live wilaya ya Temeke ,Jijini Dar Es Salaam.
Mama Tunu Pinda (wa Kwanza Kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja wa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi Lulu Mengele wakati alipotembelea banda la PPF katika tamasha la wanawake na Akiba ambapo aliweza kujiunga na kuwa mwanachama mpya wa PPF kupitia mfuko wa kuchangia kwa hiyari katika tamasha la wanawake na akiba linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Dar Live jana.
Mama Tunu Pinda (wa Kwanza Kushoto) akimsikiliza kwa makini Meneja wa Mahusiano na Masoko wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi Lulu Mengele wakati alipotembelea banda la PPF katika tamasha la wanawake na Akiba ambapo aliweza kujiunga na kuwa mwanachama mpya wa PPF kupitia mfuko wa kuchangia kwa hiyari katika tamasha la wanawake na akiba linaloendelea kufanyika katika ukumbi wa Dar Live jana.
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Tunu Pinda na wake wa Viongozi mara baada ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF kupitia mfumo wa kuchangia kwa hiyari wakati walipotembelea banda la PPF katika Tamasha la Wanawake na Akiba.
Mama Tunu Pinda akiagana na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Bi Linda Njolay mara baada ya kumaliza kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF wakati alipotembelea banda la PPF.
Mama Asha Bilali akijaza fomu ya kujiunga na PPF wakati alipotembelea banda la PPF kwenye Tamasha la Wanawake na Akiba ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo.
Afisa wa Mfuko waa Pensheni wa PPF Bi Linda Njolay akimpatia maelezo ya kujiunga na PPF Mkazi wa Jiji la Dar wakati alipotembelea banda la PPF kwenye tamasha la wanawake na akiba.
Meneja Mahusiano na masoko wa mfuko wa pensheni wa PPF Bi Lulu Mengele akiwapatia maelezo ya kujiunga na PPF washiriki waliotembelea banda la PPF.

No comments: