Mwanamke mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Rashushi Amani
Shembusho, mkazi wa Pasua, wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro,
ametapeliwa kiasi cha shilingi milioni 5.4 na watu wasiojulikana
asubuhi ya leo, Februari 20.
Bi. Shembusho akilia kwa uchungu baada ya kudangasnywa na watu wawili,
wa kike na wakiume ambao majina yao bado hayajafahamika. watu hao
walimpeleka katika Hoteli maarufu mjini moshi, Fresh Coach na
kumtapeli shilingi milioni 5.4 ambazo alikuwa ametoka kutoa Benki ya
Uchumi ya mjini Moshi.
Askari wa Hoteli hiyo inayodaiwa kutumika kumtapeli mwanamke huyo
akimtuliza Mama huyo ambaye alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo.
Mama akilia kwa uchungu.
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka
Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.
Mama akisimulia tukio zima kwa wananchi waliofika katika eneo la tukio
baada ya kumsikia akipinga ukunga kuomba msaada.
Msamaria Mwema aliyefika katika eneo la tukio na kujitolea kumpeleka
Mwanamke huyo katika kituo cha Polisi cha Kati cha Mjini Moshi.
Bi. Shembusho akipanda gari la Msamaria Mwema aliyejitolea kumpeleka
Polisi kutoa taarifa hizo.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
No comments:
Post a Comment