Saturday, February 1, 2014

Kamati ya Ardhi,Maliasili na Mazingira watembelea hifadhi ya taifa ya Mkomazi.

 Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi maliasili na mazingira Mh James Lembeli akiwa ameongozana na naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Mahamud Mgimwa wakisalimiana na wafanyakazi wa hifadhi ya Taifa ya
Mkomazi.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, maliasili na mazingira wakitembelea eneo la mradi wa kufuga faru pamoja na Mbwa Mwitu.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi,maliasili na mazingira,pamoja na viongozi wa hifadhi ya taifa ,TANAPA wakimsikiliza Mkurugenzi wa shirika la WTPF,  linalosimamia mradi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Mkomazi,Tony Fitzjohn (Kushoto)
 Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira James Lembeli akiteta jambo na Mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn kabla ya kuembelea eneo maalumu linalotumika kuhifadhi Faru.
 Mwenyekiti wa kamati ya Ardhi ,maliasili na mazingira, James Lembeli,Mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn,Naibu waziri wa maliasili na utalii  Mahamud Mgimbwa wakiwa kwenye gari maalumu tayari
kwenda kujionea mradi wa Faru.
 Mbwa mwitu wakiwa wamehifadhiwa katika maeneo maalumu ndani ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi kabla ya kuachiwa kwenda porini.
 Mbwa mwitu wakiwa wamehifadhiwa katika maeneo maalumu ndani ya hifadhi ya taifa ya Mkomazi kabla ya kuachiwa kwenda porini.
 Baadhi ya vifaa ambavyo vimekuwa vikitumika katika mradi wa Faru katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi ambavyo ni sehemu ya vinavyodaiwa kutozwa kodi  na serikali licha ya kwamba hutumika katika mradi wa Faru ambao pia ni wa serikali.

 Naibu waziri wa maliasili na mazingira ,Mahamud Mgimwa akiwa amemshika mtoto wa Tembo katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi,wengine ni mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na Mazingira James Lembeli na
mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn. 

Naibu waziri wa maliasili na mazingira ,Mahamud Mgimwa akiwa amemshika
mtoto wa Tembo katika hifadhi ya taifa ya Mkomazi,wengine ni
mwenyekiti wa kamati ya Ardhi,maliasili na Mazingira James Lembeli na
mkurugenzi wa shirika la WTPF, Tony Fitzjohn. Picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

2 comments:

Anonymous said...

Bw Michuzi nakuomba uirushe hii comments tafadhali sana Mimi binafsi nikiwa mdau wa Utalii nasikitika sana nikiona hawa wenzetu wageni ambao eidha wanafanya tafiti au uwekezaji wanapojua wanakutana na viongozi wa juu wa serekali huwa wanaonyesha utovu wa adabu wa hali ya juu kwa mavazi yao tulisha wahi kufanya mkutano na wa ziri wa utali pale Mount Meru enzi za Mama Meghji nilisha ngaa kuona hawa jamaa wakiinga kwenye mkutano na kaptura na kanda mbili sasa huyu Tony ange vaa t shirt yenye mikono inge mpa tabuu gani kwa kifupi tafsiri yangu ni dharau juu ya viongozi wetu. Swali Je angekua huyu Tony ni mwafrika mwenzetu tusingeona hilo??? kwamba ni dharau, wakati umefika wakubadilisha muono wetu juu ya mavazi turudi kwenye mila ili tuweze heshimika.

Pascal Bacuez said...

Acha upuuzi wako, Anonymous, kauli yako haina maana yoyote hapo. Kwanza bwana huyo, yaani mzungu, si kigogo wala kibosile, wala mla rushwa, wala fala ya wizara. Yeye ni msomi wa mambo ambayo hata wewe mwaafrika huna habari nayo. Wewe mwenyewe utashindwa kufuatana naye porini ili kupima na kusoma mazingira anayofahamu mzungu huyu kwa kina, tena kuliko wewe ambaye ukivamiwa na mbu utaomba kujihami katika gari yako. Halafu, unajidai kwamba bwana huyo hana heshima ; sawa, lakini je, kujiheshimu ni kuvaa vazi maalumu, au kuimudu lugha uliyozaliwa nayo ? Mboni hujui hata kutumia sentensi zifaazo katika posti yako ? Aidha, unajidai kujiheshimu ilhali wewe mwenyewe hujajitambulisha ?