Uongozi wa shirika la reli TRC Dodoma umeagizwa kuwagharamia abiria wake waliokwama station ya Dodoma huduma za chakula na nyingine muhimu kwa kipindi chote watakaposubiria kukamilika kwa matengenezo ya njia ya reli eneo la godegode mpwapwa na hatimae abbiria hao kuendelea na safari yao kuelekea Dar es salaam.
Kwa mujibu wa abiria hao waliokwama station ya Dodoma wameelezea kuwa walikata tiketi ili kuondoka Kigoma januari 2 lakini walikwama mpaka Jumanne januari 7 sababu kubwa ikiwa ni kupata hitilafu kwa treni ya mizigo kwenye njia ya reli hivyo na hatimae kufika Dodoma Januari 9 asubuhi ambapo uongozi wa TRC Dodoma uliwafahamisha kuwa kuna tatizo la kuharibika kwa njia ya reli eneo la Godegode, Mpwapwa, hivyo watasubiri mpaka jioni ya leo ndipo waendelee na safari ya Dar es salaam.
Hayo yalibainika leo wakati abiria hao waliokwama walipoandamana hadi ofisini kwa mkuu wa mkoa Dodoma kuonana naye na kuelezea adha wanayopata baada ya kukwama kwa safari yao ikiwa ni pamoja na kuingia gharama kubwa ya chakula, huduma nyingine muhimu kwenye vituo walipokwama na wengine wanawatoto na wagonjwa na hadi sasa wameishiwa kabisa fedha.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa dodoma, amewaagiza TRC Dodoma kuwagharamia chakula na huduma hizo muhimu mpaka watakapoendelea na safari yao kuelekea Dar es salaam.
Aidha Dr. Nchimbi ameelezea kuwa eneo hilo la Godegode lina tabia ya kutiririsha mikondo mikubwa na yenye nguvu ya maji yanayokusanyika kutoka milimani na hata meneo ya mikoa ya jirani kama.
Kwa upande wake mhandisi mitambo wa TRC Dodoma bw. John Mandalu amesema kazi ya marekebisho ya eneo la Godegode lililoharibika inaendelea vizuri, na itakamilika jioni ya leo na safari itaendelea na kuwa kwa muda wote wa kusubiri huduma kurejea TRC itagharamia huduma za chakula na nyingine muhimu.
Taarifa zilizopatikana ofisi ya mkuu wa wilaya ya Dodoma zinasema kuwa hadi kufikia jioni ya Leo matengenezo ya njia ya njia ya reli yalikuwa yameshakamilika na safari itaendelea kama ilivyopangwa kuendelea jioni
Abiria waliokwama Mkoani Kigoma tangu januari 2 na hatimaye leo kufika Dodoma na kukwama tena baada ya kuharibika kwa njia ya reli eneo la Godegode mpwapwa wakichaguana wawakilishi wao wa kwenda kuzungumza na mkuu wa Mkoa Dodoma kumweleza adha wanayopata asubuhi ya leo walipokwenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa kwa maandamano, pembeni ni askari wa kulinda ulinzi na usalama.
Wasafiri wawakilishi wa treni ya kati waliokwama station ya dodoma wakipeana mrejesho na wenzao juu ya kile walicho kubaliana na mkuu wa Mkoa Dodoma mara baada ya kumaliza kuzungumza naye.
Mkuu wa Mkoani dodoma Dr. Rehema Nchimbi akizungumza na abiria wa treni ya kati waliokwama Mkoani Kigoma tangu januari 2, na kukwama tena Leo Mkoani dodoma mara baada ya kuwasili Mkoani humu kufuatia uharibifu wa njia ya reli, vilevile mkuu huyo wa mkoa amewaagiza uongozi wa shirka la reli mkoani Dodoma kuwagharamia kwa huduma ya chakula na nyingine muhimu mpaka watakapoendelea na kumalizia safari yao.
Wawakilishi wa abiria wa treni waliokwama mkoani dodoma (watatu walioko kulia) walioteuliwa kwenda kuonana na mkuu wa mkoa wa dodoma kuelezea adha wanayopata baada ya kukwama kwa safari yao wakisikiliza maelekezo ya mkuu wa Mkoa wa dodoma (hayupo pichani) mapema leo, wengine kushoto ni maafisa wa jeshi la polisi Dodoma.
No comments:
Post a Comment