Friday, January 24, 2014

MKUU WA WILAYA MOROGORO AKAGUA MAONYESHO YA UJASIRIAMALI YA VIJANA WA MOROGORO

Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kukagua maonyesho ya vijana wajasiriamali ya mkoa wa morogoro akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni iliyoandaa maonyeshi hayo Ndugu Jackson Audiface. Maonyesho hayo ambayo yapo katika mpango wa kupunguza ukosefu wa ajira kwa vijana ujulikanao kama Tanzania Youth Entrepreneurship Programme (TAYEP)  ambao upo chini ya kampuni ya AJ IT Development Company Ltd.
 Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akikagua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali kutoka mkoa wa morogoro. baadhi ya vijana hao kutoka chuo kikuu cha kilimo Sokoine, Chuo kikuu Mzumbe, Chuo kikuu cha kiislaam Morogoro. Lengo la maonyesho hayo ni kuzitangaza na kuzitafutia masoko kazi za vijana wajasiriamali. 
 Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi katika meza kuu akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni iliyoandaa maonyeshi hayo Ndugu Jackson Audiface (aliyevaa shati jeupe) pamoja na mwenyekiti wa kikundi cha vijana wajasiriamali wa morogoro kijulikanacho kama MOMUYO ndugu Alexander Jokonia (wa pili kutoka kulia) pamoja na afisa tarafa wa manispaa ya morogoro Mh Pakala Pakala (wa mwisho kulia).
 Baadhi ya washiriki mbalimbali kutoka vyuo na vikundi mbalimbali vya wajasiriamali kutoka mkoani morogoro walioshiriki katika maonyesho hayo .

Mwakilishhi wa serikali ya wanafunzi kutoka chuo kikuu Mzumbe Ndugu Norbert Kabendera akitoa neno la shukrani wakati wa maonyesho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akizindua tovuti ijulikanayo kama MATUKIO NA VIJANA itakayokua ikiripoti masuala ya kijamii hususani masuala ya vijana, akisaidiwa na Mkurugenzi wa Utawala na Mipango wa kampuni ya AJ IT Development Company Ndugu Fasali Mwenzegule. Pamoja na uzinduzi huo Mkuu wa wilaya alizindua mitandao mbalimbali ya kijamii itakayotumika katika mpango huu ikiwemo akaunti katika Instagram (@youth_entrepreneurship), twitter (@youth_entrepreneurs) na facebook (Tanzania-YOUTH-Enterprenuership).

 Mkuu wa wilaya ya Mororgoro Mh Said Ally Amanzi akitoa hotuba mara baada ya kukagua maonyesho hayo ambapo aliomba taasisi za fedha kupunguza riba kubwa za mikopo hasa kwa vijana wanaojiajiri pamoja na hilo aliomba makampuni mengi kujitokeza kuwezesha mpango kufanyika nchi nzima ili uweze kuwafikia vijana wengi zaidi Tanzania.

Na Fasali Mwenzegule

Tanzania Youth Entrepreneurship Programme (TAYEP) ni mpango ulianzishwa na kampuni ya AJ IT Development Company kwa lengo la kuwasaidi vijana ambao hawana  ajira kuweza kujiajiri kwa kuwa wajasiriamali.

Mpango huu uliobuniwa mwaka 2013 umewawezesha vijana 50 kutoka mikoa ya Arusha na morogoro kujiajiri kwa njia ya kilimo, Utalii na  ubunifu wa kazi za mikono. Lengo la mpango huu ni kutangaza na kuzitafutia masoko kazi za wajasiriamali, kutoa elimu kuhusu ujasiriamali kwa vijana ambao hawajiajiri, kuibua miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kushirikiana na vijana kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.

Mkakati iliyowekwa na kampuni hiyo kwenye mpango huu ni kupeleka maonyesho haya mikoa yote Tanzania kwa lengo la kuwafikia vijana wengi zaidi ambao bado hawajiajiri.

Changamoto kubwa zinazoukabili mradi huu ni ukosefu wa rasilimali fedha ambao unasababisha vijana wengi kukosa fursa hii, tunawaomba wadau mbalimbali wa vijana kujitokeza kusaidia mradi huu kuwafikia vijana wengi zaidi ili kuwasaidi vijana wengi kupata ajira na nchi iweze kupiga hatua kubwa kwenye maendeleo na kutimiza kauli mbiu ya matokeo makubwa sasa yaani "BIG RESULT NOW". 

No comments: