Wachezaji wa gofu wa kulipwa walioshiriki mashindano ya Gofu ya
NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na
wadhamini wa mashindano hayo kwa upande wa Profesionals ambao ni ORYX
Energies Ltd.Mwenye t-shirt nyekundu kwa waliochuchumaa ni mkurugenzi
wa kampuni ya Oryx,Chris Swat na aliyesimama mwenye t-shirt nyekundu
ni mwakilishi wa mauozo wa kampuni ya Oryx kanda ya kaskazini Edga
Mhagama.
Wacheza wa gofu wa ridhaa walioshiriki mashindano ya Gofu ya NSSF,ORYX
Tanzania Open 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa
mashindano hayo kwa upande wa Armature ambao ni shirika la hifadhi ya
jamii la NSSF.
Baadhi ya maofisa kutoka NSSF mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia
shughuli ya kukabidhi zawadi kwa washindi katika mashindano ya gofu ya
NSSF,ORYX Tanzania Open 2013.
Afisa mtndaji utawala wa kiwanda cha sukai cha TPC akizungumza jambo
wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi wa michuano ya Gofu ya
NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 iliyofanyika katika viwanja vya gofu vya
TPC.
Afisa operesheni wa shirika la hifadhi ya jamii NSSF mkoa wa
Kilimanjaro Daudi Mwangole akizungumza jambo wakati wa kukabidhi
zawadi kwa washindi wa michuano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open
2013 iliyofanyika katika viwanja vya gofu vya TPC.
Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro Faisal Issa akimwakilsiha mkuu wa
mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama katika utoaji wa zawadi kwa washindi
wa michuano ya Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 iliyofanyika
katika viwanja vya gofu vya TPC.
Mkurugenzi wa kampuni ya ORYX,Chris Swat akifurahia jambo na mshindi
wa mashindano ya gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 kwa upande wa
wachezaji wa kulipwa Yasin Saleh.
Mkurugenzi wa kampuni ya ORYX,Chris Swat akikabidhi zawadi ya jiko
pamoja na mtungi wa gesi kwa mmoja washiriki wa michuano ya gofu ya
NSSF,ORYX Tanzania Open 2013 waliofanya vizuri kwa wenye umri juu ya
miaka 55.Vicent Maguu.
Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa ridhaa katika mashindano ya gofu ya
NSSF,ORYX Tanzania 2013,Frank Roman akikabidhiwa kikombe na katibu
tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Faisal Issa,katikati ni mwakilishi wa
wadhamini wa mashindano hayo NSSF,Daudi Mwangole.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
MASHINDANO makubwa ya mchezo wa Gofu ya NSSF,ORYX Tanzania Open
yamemalizika juzi katika viwanja vya TPC mkoani Kilimanjaro huku
ikishudiwa mchezaji Yasin Salehe wa klabu ya Dar es salaam Gymkhana
akishika nafasi ya kwanza kwa upande wa wachezaji wa kulipwa baada ya
kupiga mikwaju 302.
Saleh alifanikiwa kujinyakulia kitita cha fedha kilichotolewa na
kampuni ya ORYX ambao ndio walikuwa wadhamini kwa upande wa wachezaji
wa kulipwa baada ya kuwabwaga wapinzani wake Godfrey Revelian
aliyepiga mikwaju 303 na Hassani Kadio aliyeshika nafasi ya tatu kwa
kupiga mikwaju 308.
Nafasi ya nne kwa upande wa wachezaji wa kulipwa ilichukuliwa na
mchezaji John Davies wa klabu ya gofu ya Mombasa baada ya kupiga
mikwaju 309 huku nafasi ya tano ikichukuliwa na Salim Dilunga
aliyepiga mikwaju 310 na nafasi ya sita kwa washindi walipewa zawadi
ni Salim Mwanyenza aliyepiga mikwaju 312.
Upande wa wachezaji wa gofu wa ridhaa waliodhaminiwa na mfuko wa
hifadhi ya jamii NSSF,mshindi wa kwanza alikuwa ni Frank Roman
aliyepiga mikwaju 293 akifungana na mpinzani wake Ally Mcharo
aliyeshika nafasi ya pili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mchezaji
Nuru Morel aliyepiga mikwaju 294.
Wasindi wengine na mikwaju waliyopigwa kwenye mabano ni Abas Adam(297)
aliyeshika nafasi ya nne,Abdala Yusuph (301)aliyeshika nafasi ya tano
huku Jimmy Morel (306) akishika nafasi ya sita.
Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, katibu tawala
mkoa wa Kilimanjaro Faisal Issa alisema serikali mkoani Kilimanjaro
itaendelea kusaidia michezo mbalimbali ukiwemo mchezo wa gofu ili
kuweza kupata wachezaji watakao wakilisha taifa katika mashindano
mbalimbali.
“Rai yangu ni kwamba tusifikirie kuanza kucheza mchezo huu wa gofu
tukiwa ukubwani…ni vema tukafikiria kuanza kuwalea vijana katika
mchezo huu ambao wakifika umri mkubwa ni wazi watakuwa ni wachezaji
wazuri na ambao watatuwakilisha vyema.”alisema Issa.
Alisema mkoa wa Kilimanjaro umeweka mikakati ya kurejesha hali ya
michezo katika mkoa kwa kuundwa kamati maalumu ambayo itakuwa na
wajibu wa kufanya vikao vya kuangalia miechezo inaendaje hasa kwa
kushirikisha vyama vya michezo.
Naye katibu wa chama cha mchezo wa Gofu nchini (TGU)Mohamed Sadick
aliipongeza kampuni ya TPC pamoja na wadhamini wa mashindano hayo
shirika la hifadhi ya jamii NSSF pamoja na kampuni ya Oryx Energizer
kwa kufanikisha mashindano hayo makubwa ya gofu nchini.
“Suala la kushirikisha Professionals ni jema sana kwani wachezaji
chipukizi wanajifunza kutoka kwao kwani tunajenga gofers wazuri ambao
wanajua sheria na hili lazima tuendelee kulisisistza kila atakaye
andaa mashindano ashirikishe pia Professionals ili kusaidia viwango
vya vijana wetu”alisema Sadick.
Kwa upande wake afisa utawala wa kiwanda cha sukari TPC Jafary Ally
alisema kampuni ya TPC imeendelea kufanya ukarabati wa maeneo
mbalimbali ya uwanja wa gofu ili uweze kuwa na kiwango kinachotakiwa
kimataifa.
No comments:
Post a Comment