Sunday, December 29, 2013

Rais Shein wa Zanzibar katika Mahafali ya 9 ya Chuo Kikuu cha Taifa SUZA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamuhuna,wakati alipowasili Chuo Kikuu cha Taifa,kampasi ya Tunguu,katika sherehe za mahfali ya 9 ya chuo hicho,ambayo wahitimu wa fani mbali mbali wamepatiwa Shahada,Stashahada na Vyeti.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,akisalimiana na walimu wa Chuo Kikuu cha SUZA,alipowasili katika mahfali ya 9 yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja, leo.
Baadhi ya wahitimu wa fani mbali mbali wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,wakiwa katikaa maandamano wakati wa sherehe za mahfali ya 9 chuo hicho,yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja, leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,(wa pili kulia) akiongoza maandamano wakati wa sherehe za mahfali ya 9 chuo hicho,yaliyofanyika kampasi ya Chuo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja leo,yaliyowashirikisha baadhi ya wahitimu na walimu.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya sayansi ya kompyuta,ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar,wakisimama walipotunukiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,(hayupo pichani) katika mahafali ya 9 iliyofanyika kamapasi ya Tunguu leo.
Baadhi ya wahitimu wa shahada ya sayansi na Elimu,ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar,baada ya kutunukiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,(hayupo pichani) katika mahafali ya 9 iliyofanyika kamapasi ya Tunguu leo.
Wahitimu wa Stashahada ya Teknolojia ya habari,waliotunukiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti waa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA,(hayupo pichani) katika mahafali ya 9 iliyofanyika kamapasi ya Tunguu leo,(kutoka kushoto) Stewat Njelekela,Seif Mohamed Nassor na Husna Shaabani Bwamadi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments: