Waumini wa kanisa katoriki Parokia ya Maonano, Mawela wakiwa katika ibada.
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akitembelea ukumbi wa kisasa
unaojngwa katika Parokia hiyo kwa ajili ya shughuli mbalimbali.
Baadhi ya waumini pamoja na wageni mbalimbali waliojitokeza katika
harambee ya ujenzi wa ukumbi wa kisasa katika Parokia ya Maonano
Mawela.
Mshereheshaji wa shughuli hiyo ya harambee ya ujenzi wa Ukumbi wa
kisasa Godwin Gondwe akijaribu kuweka mambo sawa .
Paroko wa parokia ya Maonano ,Mawela Padre Anthony Marunda akisoma
risala kwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia ujenzi wa ukumbi
wa kisasa katika kanisa hilo.
Waziri mkuu mstaafu Fredrick Sumaye akizungumza katika harambee ya
ujenzi wa ukumbi wa kisasa wa kanisa katoliki Parokia ya Maonano
Mawela jana.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye pamoja na mshereheshaji wa shughuli hiyo
Godwin Gondwe wakijadiliana jambo na mmoja wa wajumbe wa kamati ya
harambee ya Ujenzi wa ukumbi huo wa kisasa Anthony Komu.
Waziri mkuu mstaafu Sumaye akimkaribisha Mbunge wa jimbo la Moshi
vijijini Dk Cyril Chami kuchangia katika harambee ya Ujenzi wa Ukumbi
wa kisasa katika kanisa katoliki Parokia ya Maonano Mawela .
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye amesema kuwa mwaka 2014 ni mwaka
muhimu sana kwa mustakabali wa taifa letu kwa sababu ni mwaka wa
uchaguzi katika ngazi za serikali za mitaa na ni mwaka wa maandalizi
ya uchaguzi mkuu mwaka 2015, hivyo watanzania wamwombe Mungu awajalie
hekima na busara, na kuwapa ujasiri waweze kuchagua viongozi
watakaofaa kuongoza kwa hekima, busara, upendo na haki.
Akizungumza na Mamia ya Waumini mbalimbali waliojitokeza katika
harambee ya kuchangia ujenzi wa Ukumbi wa Parokia ya Maonano, Mawela
katika Jimbo Katoliki la Moshi Sumaye alisema ni ukweli ulio wazi kuwa
chaguzi za kitanzania sasa zimegubigwa na rushwa na vishawishi vingi
wala siyo ubora, uhodari wala tabia ya anayetaka nafasi ya uongozi.
“Hivi sasa rushwa na matumizi makubwa ya fedha za kuwanunua wapiga
kura vinataka kuwa utaratibu halali wa kuwapata viongozi wetu wa ngazi
zote kuanzia ngazi za vijiji na mitaa hadi ngazi ya Urais, utaratibu
huuu ni wa hatari na lazima tuupige vita kwa pamoja” alisema Sumaye.
Aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuwa wacha Mungu, watu wa kweli,
wenye kuchukukia mapato ya udhalimu, hao ndio wanaweza kuwa viongozi
kwa kutegemea uwezo wao, upeo wao, uhodari wao, ujasiri wao na
uaminifu wao kwa Mungu na kwa jamii wanayoiongoza.
Sumaye alisema pia, Katika utaratibu wa demokrasa sahihi na halisi,
wapiga kura hutakiwa kuwachagua viongozi kufutana na sifa nzuri za
uongozi alizo nazo, na kuonya kuwa Kiongozi anatafutwa na jamii na
siyo yeye kusaka uongozi, mbaya zaidi ni pale msaka uongozi
anapotafuta nafasi hiyo kwa njia zisizofaa kama vile rushwa na kununua
wapiga kura.
“Uongozi hautafutwi kwa udi na uvumba wala kwa rushwa, leo chaguzi
zetu zimegubikwa na rushwa na vishawishi vingi na siyo ubora, uhodari
wala tabia ya anayetaka nafasi ya uongozi, rushwa na matumizi makubwa
ya fedha kununua wapiga kura vinataka kuwa utaratibu wa kawaida tena
halali wa kuwapata viongozi wa ngazi zote kuanzia kijiji hadi Urais,
huu ni utaratibu wa hatari na lazima upigwe vita kwa pamoja” aliongeza
Sumaye.
Sumaye akinukuu Biblia takatifu (Kut.23:8) inayosema “nawe usipokee
rushwa kwani rushwa huwapofusha macho hao wanaonao, na kuyapotoa
maneno ya wenye haki” alionya kuwa kama Biblia inasema rushwa
inapofusha macho, sisi watanzania tukichagua kiongozi mla rushwa au
mtoa rushwa au anayenunua wapiga kura, huyo hawezi kutuongoza tufike
tunakotaka, tukichagua kiongozi wa aina hiyo atatumia nafasi yake
kujinufaisha yeye na rafiki zake.
Katika hotuba hiyo pia Sumaye alisema watu walioiba wakamatwe na
kufungwa maana wametenda jinai, hivyo hivyo waliotoa rushwa au
kuifisadi nchi, kuuza madawa ya kulevya au kuua wanatakiwa kutubu kwa
kuwa hiyo ni dhambi lakini wakikamatwa waadhibiwe maana hayo yote ni
makosa ya jinai,
Katika harambee ya ujenzi wa Ukumbi huo Sumaye alifanikiwa kuchangisha
pesa taslimu 55,295,500, na ahadi ya 170,000,000 Jumla ni milioni
225,295,500. Akivuka lengo la harambee hiyo ambayo ilikuwa imepangwa
150,000,000. Gharama halisi za Ukumbi huo wa kisasa wa Parokia ya
Mawela ili ukamilike utagharimu 450,000,000/.
No comments:
Post a Comment