Baadhi ya wachezaji wa timu ya Taifa wa ngumi za Ridhaa pamoja na wadau wengine wa mchezo huo wakati wa hafla hiyo katika hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam
Aliyesimama kushoto ni mkurugenzi wa Afrika Mashariki kupitia kinywaji cha Battery Bwana Tony Misokia akiwa anaongea na wananchi walioshiriki katika Hafla hiyo. Aliyesimama kulia ni Bw. Mfugale, Mkurugenzi Mkuu wa Peacock hotel
Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) Bw. Lukelo Anderson akiwa sambamba na Afisa habari wa Ngumi za ridhaa Tanzania Bwana Salum Viduka wakati wa Hafra hiyo.
Hawa ni Baadhi ya wachezaji wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF)
Wa kwanza kulia ni Nahodha wa Timu ya Taifa ya Ngumi za ridhaa Tanzania bwana Nassari Mafuru
Kutoka kushoto aliyevaa shati jeupe ni Bwana Anthony Mwang'onda ambaye ni mjumbe wa mashindano na vifaa wa Shirikisho la Ngumi za ridhaa Tanzania (BTF) akiwa na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Bwana Hassan Mzonge
Shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania limefanya hafra
fupi iliyo jumiisha wachezaji wa ndondi , makocha wadau na Vyombo vya habari
kwaajiri ya kuendeleza kuweka mshikamano wa kuweza kuwainua vijana ambao bado
hawajaweza kupata ajira kuweza kujiunga
na shilikisho la ngumi za ridhaa Tanzania.
Shilikisho hilo ambalo limeanzisha mashindano ambayo yanatambulika kwa jina la PSPF Boxing Award sambamba na waandaaji
wa Hafla hiyo wakiwa ni wadhamini wa mashindano hayo iliyofanyika katika eneo la (CnG) ambapo waliweza kudhamini kwa
kuandaa chakula cha usiku kwa ajili ya kuendelea kuweka mahusiano baina ya
washiriki wote wanao shiriki katika kuendeleza mchezo wa ngumi Tanzania
Akizungumzia lengo la kuweka hafla hiyo Afisa habari wa
shirikisho la ngumi Tanzania Bw.Salum Kuhowa Viduka amesema "Tunawaomba
wanajamii kuweza kutupa ushirikiano kwa muda wote ambao mashindano haya yanapo
kuwa yana wasili katika miji,wilaya,manispaa,na nk kuweza kujitokeza kwa wingi
ili kuona jinsi fursa kwa vijana zinavyo patikana kupitia mchezo wa ngumi za Ridhaa"
Mwisho Makamu Rais Bw.Lukelo
Andason alifunga hafla hiyo kwa kuwapongeza watu wote walioweza kufika
na kujumuika pamoja ili kuendeleza kujenga umoja wa ngumi Tanzania
No comments:
Post a Comment