Monday, December 23, 2013

BODABODA DAY: ASILIMIA 90 WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI HIARI WA PSPF

Zaidi ya asilimia 90 ya waendesha bodaboda waliohudhuria tamasha la siku ya waendesha bodaboda lililopewa jina la siku ya waendesha bodaboda wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Mwanjaa Sembe amesema udhamini wao katika tamasha hilo ni moja ya mikakati yake ya kuwafikia watu mbalimbali walio kwenye sekta isiyorasmi ili wajiunge na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS).


Wakati tamasha hilo lililofanyika jumapili ya desemba 22 mwaka 2013 likiendelea waendesha bodaboda wengi walifurika kwenye banda la mfuko wa pensheni wa PSPF kujisajili na kujiunga na mpango wa hiari wa uchangiaji PSS.

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa Uendeshaji wa PSPF, January Bunetta kwa kutoa Mchango mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala, Michael Roswe akisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam.
 Watumishi wa PSPF wakitoa maelezo ya namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) kwa waendesha bodaboda waliohudhuria kwenye tamasha la siku ya bodaboda
 Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa PSPF, Mwanjaa Sembe akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu za kujiunga na PSS
Afisa mwandamizi wa fedha wa PSPF, Hidaya Mganga akimsaidia kujaza fomu mmoja wa waendesha bodaboda aliyejitokeza kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSPF
Afisa wa mpango wa uchangiaji wa hiari Mwajuma Ali akipitia fomu za usajili wakati wa tamasha hilo
Afisa wa uendeshaji PSPF, Halima Isaa akiwaelekeza namna ya kujaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS
Mtumishi wa PSPF akigawa vipeperushi kwa waendesha bodaboda vinavyoeleza namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari
Waendesha bodaboda wakisoma fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari kabla ya kujaza maelezo yao na kujisajili
Afisa fedha wa PSPF, Reginald Msafiri akigawa vipeperushi
Waendesha bodaboda wakisoma vipeperushi vya PSPF wakati wa tamasha
Afisa masoko wa PSPF, Queen Edward


Afisa Fedha wa PSPF, Mohamed Madenge akigawa vipeperushi
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo
Mh. Lowasa akiwaaga waendesha bodaboda
Watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja

No comments: