Thursday, November 28, 2013

MARUFUKU MATUMIZI YA ‘WOOD’ KWENYE SOKO LA FILAMU

·         ‘BONGOWOOD’, ‘SWAHILIWOOD’ MARUFUKU.
Na ANDREW CHALE, ARUSHA
 WAAFRIKA wametakiwa kukataa utumwa na kuiga  neno la ‘WOOD’,

kwenye soko la filamu hasa baada ya nchi nyingi kukopi  jina la ‘HOLLYWOOD’ ambalo ni eneo lililopata umaarufu mkubwa kwenye soko la filamu Duniani kwa kuwa na wasanii nyota na studio za kisasa, za masuala ya filamu.
Akielezea mapema leo kwenye semina ya waandishi wa habari za Sanaa kuhusu Filamu za Afrika, Mkurugenzi wa Tamasha la Filamu za Kiafrika la  Arusha (Arusha African Film Festival –AAFF 2013) na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Arcadia,  kilichopo Pennsylvania, Marekani , Mr. Akpor Otebele (pichani),  alisema Waafrika waache dhana ya kuendelea kutumia jina hilo ambalo nchi nyingi wamekuwa wakitumia viunganishi vya neo hilo la ‘Wood’  bila kujua maana hasa la kuendelea kulitumia.
Hii aina maana, ni la kuliacha na Nigeria kule waigizaji wengi wanatafakari maana ya hili neo lakini jibu hakuna, lakini bado wanaendelea kulitumia” alisema.
Akitolea mfano wa baadhi ya nchi zinazotumia jina hilo kutoka Hollywood, ni pamoja na : Bongowood/ Swahiliwood (Tan zania), Nollywood (Nigeria), Riverwood (Kenya), Ghollywood (Ghana), SierraWood (Sieralion)na Congowood (Kongo) na mengine mengi.
Akpor  Otebele aliongeza kuwa, kuendelea kutumia viunganishi hivyo ni kuwanufaisha watu wa Magharibi na kuupamba Mji wa Hollywood  unaoishi mastaa na studio maalufu huko Lose Angels nchini Marekani, ambapo kwa dhana hii inafanya Waafrika kuwa watu wasiojua wanachokifanya.
…”Swahiliwood, its means, Swahili ubao? Is  that sure? So why to use ‘Wood’??  in Swahili mean ‘UBAO’?? Alisema Akpor Otebele.
Na kuongeza kuwa  nchi nyingi za Afrika zinatumia neno
'Wood' kinyume na maana yake  huku wengine wakipokea misaada bila kujijua kuwa wanarubuniwa ujinga. "Kwa nini wanahitaji Bongowood. Mimi ninavyojua wood ni mbao, kwa nini wasiseme, swahili movie?" alihoji.
Otebele aliwataka wanahabari  kuwaelemisha wadau wa filamu kuwa, Hollywood si jina la kutungwa bali la mji uliotokea kuwa maarufu kutokana na kusheheni vitendea kazi bora na vya kisasa na kwenye makazi  ya wasanii nyota mbali mbali, ni wakati wa kulipinga.
Mbali na hilo, Otebele  aliwataka wasanii na waongoza filamu Afrika na kwingineko kuzingatia  filam,u za kiushindani ilikufia malengo yao.
Hii ni kwa  kuwataka kuzingatia filamu zenye ubora, maarifa na zitoazo mafunzo mbele ya jamii inayotuzunguka kila siku.
Katika semina hiyo inayofanyika  jini hapa,  katika hoteli ya  kisasa na kitalii ya Silver Palm Hotel,  ambapo mada mbali mbali  zitawasilishwa kuhusu tasnia ya  filamu barani Afrika huku  watoa mafunzo wengine wakiwemo Mtaalamu wa filamu wa chuo kikuu Mlimani, ambaye pia ni mtayarishaji wa filamu ya ‘CHUNGU’,  Shule  na  Mtendaji Mkuu wa ZIFF, Prof. Martin Mhando.
Semina hiyo ilianza mapema leo inatarajia kuendelea  hadi Desemba Mosi,  huku ikiandaliwa na Waandaji wa Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Majahazi (Zanzibar International Films Festival –ZIFF)  kwa udhamini wa Mfuko wa kusaidia Vyombo vya habari nchini  (Tanzania Media Fund-TMF)  ambapo waandishi mbali mbali wanapatiwa mafunzo juu ya uandishi wa habari za Sanaa hapa nchini kwenye vyombo vyao vya habari na mitandao ya kijamii zikiwemo blogs.
Pia semina hii inaendana na tamasha kubwa la filamu  la AAFF 2013, lililoanza  Novemba 25 hadi Desemba Mosi, kwenye  kumbi mbali mbali za Alliance Francaise, Via Via , Mount Meru Hotel, Mango Tree & New Arusha Hotel, ambapo kiingilio ni BURE/FREE ENTRY.
 
Ratiba ya Warsha ni kama ifuatavyo: -
DATE
UNIT
ACTIVITY DETAILS
EVENING
27/11/13
 
Arrival
Watch films
28/11/13
Critical Analysis
Otebele
Film Review and Analysis
A philosophical and African cinema centred approach. Include comparison of classical genre approaches to African cinema study.
Watch identified film or theatre show.
Write articles for following day
29/11/13
Critical AnalysisShule
Theatre Review and Analysis- including African traditional theatre arts and contemporary theatre practice in Tanzania. The evening will be given to mentors to work with the trainees.Techniques of writing the film review; preparation and treatment of form and content; problems, responsibilities and ethics of film reviewing.
Visit the Arusha Museum or watch films
 
Evening Class
 
Send articles to Newspapers/TV/Radio
30/11/13
Arts Coverage and Issues in Contemporary Media Culture
Mhando
Discussions on Media as a tool for knowledge creation. A philosophical and socio-political perspective. Learn about the development of online arts journalism, and how to use Weblogs, podcasts, video, and social networking to review and report on the arts. We engage with how people use the arts to share content, opinions, insights, experiences, perspectives, etc.  This workshop looks at social media culture and how it is changing the way we do business. Assessment
Send articles to Newspaper/TV/Radio
1/12/ 13
 
Departures
Send articles to Newspapers/TV/Radio
 

No comments: