Saturday, November 16, 2013

MAMA SALMA KIKWETE NA WAKE WA MARAIS WA JUMUIA YA MADOLA WATEMBELEA MAENEO MBALIMBALI MUHIMU HUKO COLOMBO-SRI LANKA

 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA,  akishangiliwa na watoto wadogo (chekechea) wa shule ya awali ya Carlton iliyoko Colombo, nchini Sri lanka wakati Mama Salma na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Madola walipotembelea shule hiyo leo tarehe 16.11.2013.
 Mama Salma Kikwete akishangiliwa na watoto wadogo (chekechea) wa shule ya awali ya Carlton iliyoko Colombo, nchini Sri lanka wakati Mama Salma na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Madola walipotembelea shule hiyo tarehe 16.11.2013.
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akizungumza na Mke wa Rais wa Sri lanka Madame Shiranthi Rajapakse ambaya pia ni Mwenyekiti wa Muungano wa Shule za Carlton nchini humo wakati walipokutana kwenye moja ya shule hizo iliyoko Colombo
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa anaingia Gangaramaya temple inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha nchini Sri lanka tarehe 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa kwa ngoma wakati alipokuwa anaingia Gangaramaya temple inayotumiwa na watu wa madhehebu ya Budha nchini Sri lanka tarehe 

 Mama Salma Kikwete akifuatiwa na Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mama Louise  Khurshid, na Mama Charlotte Scott, Mke wa Makamu wa Rais wa Zambia wakipata maelezo kuhusiana na Gangaramaya temple kutoka kwa Naibu Mkuu wa Temple hilo Van Kirinda Assage
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya vitabu kutoka kwa Kiongozi wa Gangaramaya Temple Van Kirinda Assage.


  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Madola wanaohudhuria mkutano wa Madola mjini Colombo nchini Sri lanka wwakipokewa na mwenyeji wao Mama Shiranthi  Rajapakse wakati walipotembelea Maonesho ya kazi za mikono (handcrafts) yaliyoko eneo la Janakala Kendraya katika vitongoji vya mji wa Colombo.
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa binti Dunya Liyanage, 8, anayesoma darasa la 3 katika Shule ya Msingi ya Meusnes iliyoko mjini Colombo wakati Mama Salma na wake wa Marais kutoka nchi za madola walipotembelea maonesho ya Kendraya
 Wake wa Marais na wakuu wa nchi za Jumuia ya Madola wakimwangalia  mama mmoja  wa Sri lanka aliyekuwa akitwanga kwenye kinu wakati walipotembelea maonesho ya Kendraya huko Colombo
 Mama Salma Kikwete akiwa pamoja na wake wa Marais kutoka nchi za Jumuia ya Madola wakiangalia jinsi mwanaume na mwamamke wakishirikiana kufinyanga vyungu.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Mama Louise Khurshid, Mke wa Waziri wa Mambo ya Nje wa India pamoja na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia wakitembelea sehemu mbalimbali za maonyesho Kendraya. PICHA NA JOHN LUKUWI 

No comments: