Msimamizi wa Kiwanda cha Korosho,Korosho Africa Ltd akifafanua namna ya Korosho zinavyobanguliwa kwa kutumia mashine za kisasa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,Kinana na Ujumbe wake wanamalizia ziara yao leo ndani ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kesho kuwasili ndani ya Wilaya ya Namtumbo kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo ya chama na wananchi sambamba na miradi.
Maeleoz yakitolewa namna ya Korosho zinavyochambuliwa mara baada ya kubanguliwa na mashine ya kisasa,ampapo zao hilo la biashara linalotegemewa na wakulima wa Wilaya ya Tunduru wamekuwa wakilalamikia suala la bei kuwa ndogo inayopangwa na Wanunuzi hali inayowapelekea Wakulima wa zao hilo kukata tamaa na maisha yao kuendelea kuwa duni siku hadi siku.
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Baadhi ya akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,wakiendelea na kazi yao ya kuchambua Korosho,ambapo imeelezwa kuwa mtu mmoja huchambua korosho kwa wastani wa kilo kumi mpaka 15.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,akizungumza na akina mama wanaofanya kazi ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa mapema leo mchana walipokwenda kutembelea kiwandani hapo na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo.
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akizungumza na akina mama wanaofanya kazii ya kuchambua Korosho ndani ya kiwanda cha Korosho Africa,ambao baadhi ya akina mama hao walilamika suala la ujira wanaolipwa kuwa ni mdogo na haukidhi mahitaji yao ya kila siku.
Uchambuzi wa Korosho ukiendelea.
Tahadhari ya maandishi ndani ya kiwanda cha Korosho kwa wafanyakazi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa tarafa ya Jakika mapema leo mchana,ikiwa sambamba na kuweka jiwe la msingi kwenye Ofisi ya CCM ya kata ya Jakika,Wilayani Tunduru mkoani Ruvuma,Ndugu Kinana ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi nje ya Zahanati ya kijiji cha Matemanga,Ndugu Kinana aliweka jiwe la msingi nyumba mbili za Waganga ikiwemo na kushiriki ujenzi wa mradi wa nyumba hizo akiwa sambama na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Moja ya nyumba za watumishi wa Zahanati ya kijiji cha Matemanga ambayo Ndugu Kinana aliweka jiwe la msingi.
Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana sambamba na ujumbe wake Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro,wakishiriki ujenzi wa nyumba mbili za Waganga katika zahanati ya Matemanga wilayani Tunduru mkoani Ruvumma.
Baadhi ya akina mama wakifurahia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake Wilaya ya Tunduru mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Sehemu ya wakazi wa Tunduru mjini wakishangilia jambo wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.
Pichani kulia Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihitimisha ziara yake mapema leo jioni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Baraza la Iddi,Wilayani Tunduru mkoani Rukwa na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu.Kinana na Ujumbe wake kesho ataelekea Wilayani Namtumbo kuendelea kukagua miradi ya mbalimbali ya Wananchi na chama kwa ujumla.
Baadhi ya Mafundi wakiendelea na ujenzi kwenye moja ya darasa ikiwe ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa madarasa na maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Mgomba,ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro walishiriki ujenzi -
Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrhman Kinana akiwa ameambatana na ujumbe wake,Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakiishiriki ujenzi kwenye moja ya darasa ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa madarasa na maabara katika shule ya sekondari ya kata ya Mgomba,iliopo Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.Anaeshuhudia ni Mkoa wa Ruvuma,Mh Said Thabit Mwambungu.
No comments:
Post a Comment