Monday, November 25, 2013

KINANA AANZA ZIARA RASMI WILAYANI KYELA,LEO KUUNGURUMA WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ipinda wilayani Kyela kwenye mkutano wa hadhara ambao ndio mkutano wake wa kwanza kama Katibu Mkuu wa CCM lakini pia ndio siku aliyowasili akitokea Ruvuma .
 Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimu wakazi wa Ipinda wilaya ya Mbeya na kuwasihi wakina mama wawe mstari wa mbele kuhakikisha mabinti zao wanapata elimu.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Ipinda na kuwaeleza mambo muhimu ya kutafakari kabla hajakurukupia siasa na baadhi ya vyama vingi vipo kwenye mfumo na utawala binafsi.
 Mbunge wa Kyela Dk. Harisson Mwakyembe akihutubia wakazi Ipinda wa kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amekaa Nyumbani kwa Balozi wa Nyumba 10 Ndugu Menas Ndoma .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa  na ndugu waliokuwa wanachama wa CHADEMA ambao wamerudisha kadi zao kama waonekanavyo pichani na kujiunga na CCM,kushoto ni mtoto Raphael Simon na Baba yake Simon Raphael wa pili kulia pamoja na jirani yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza  na Wananchi wa Shina namba 1 kata ya Walema,alipokwemda kumtembelea Balozi Menas Ndoma.
Wananchi wa Shina namba 1kata ya Walema wakishangilia salaam za Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokwenda kumtembelea Balozi Menas Ndoma wa kata ya walema.

No comments: