Thursday, October 17, 2013

MBUNGE KABATI AMWAGA MISAADA JIMBO LA IRINGA MJINI

 Mbunge  wa  viti maalum  mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati  akitolea  ufafanuzi misaada  aliyoitoa

" Nitaendelea  kuwa karibu na wana  Iringa pale  mtakapohitaji msaada  wangu  nitatoa  kupitia  posho yangu"
 Mbunge  Kabati  akikabidhi  maada wa  vitabu vya masomo mbali mbali kwa  wakuu wa shule za  sekondari  jimbo la Iringa mjini


 Mbunge Kabati akikabidhi msaada wa madawati kwa  walimu  wakuu wa shule za msingi jimbo la Iringa mjini katikati mwenye kanzu ni kamanda wa UVCCM mkoa  wa Iringa  Salim Asas


Katibu  wa chama  cha  waandishi wa habari  mkoa wa Iringa Bw  Francis Godwin akipokea  msaada wa  kompyuta   kutoka kwa mbunge Ritta Kabati  jana







Na  Francis Godwin Blog
MBUNGE  wa  viti maalum  mkoa  wa  Iringa Ritta  Kabati  ametimiza ahadi yake  ya  madawati 100,vitabu kwa  shule za msingi na  sekondari  pamoja na kompyuta moja  kwa  klabu ya  waandishi  wa habari  mkoa  wa Iringa (IPC)

Akikabidhi  ahadi  hiyo jana  kabati  alisema  kuwa  amelazimika  kutimiza ahadi hiyo  ili  kupunguza sehemu ya ahadi  mbali mbali ambazo alipata  kuwaahidi  wananchi wa  jimbo la Iringa mjini pamoja na zile ambazo aliombwa na  wanahabari  mkoa  wa Iringa  ili  kusaidia kuongeza vitendea kazi kwa ofisi ya wanahabari mkoani hapa.

Kabati  alisema  kuwa madawati  hayo  100 aliyokabidhi ni kwa shule  za msingi nane  za jimbo la Iringa mjini na vitabu ni kwa ajili ya  shule za sekondari 5  za jimbo la Iringa mjini.

Mbunge  huyo alisema  madawati hayo yanathamani ya  zaidi ya  Tsh  milioni 6  wakati  vitabu  hivyo ameviomba kutoka kwa  wadau  wake  kwa ajili ya kusaidia  kupunguza uhaba  wa  kiada na ziada katika  shule za sekondari   jimbo la Iringa mjini.

Hata  hivyo alisema  kuwa misaada  hiyo amekuwa akiitoa  mfukoni  mwake na posho yake anayoipata  bungeni hasa  ukizingatia yeye  si mbunge wa  jimbo ambae  anapewa bajeti  ya  kusaidia maendeleo  ya jimbo kwa maana ya  mfuko wa maendeleo  wa jimbo .

" Mimi  nimekuwa  nikitumia posho  zangu  kusaidia maendeleo  jimbo la Iringa mjini hasa mkitambua kuwa  mimi  sina mfuko  wa jimbo ila kama ningelikuwa mbunge wa  jimbo kero  hizi  zingetatuliwa  kupitia mfuko wa  jimbo.....ila  bado nahawakikishieni  nitaendelea  kuchangia maendeleo ya  jimbo la Iringa mjini"

Akielezea  juu ya msaada wake wa kompyuta kwa  aliyoikabidhi kwa uongozi wa IPC  Kabati  alisema  kuwa  mbali ya msaada  huo wa Kompyuta  bado ataendelea  kuwasaidia  wanahabari  Iringa  ikiwa ni pamoja na kumwomba  waziri  wa habari , vijana utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangala  ili  ikiwezekano IPC  kuendelea  kusaidia   zaidi  hasa kupitia IPC Vicoba  mpango ambao  umekuwa  ukiwasaidia  wanahabari  kupata  mikopo  nafuu

Kwa  upande  wake mlezi  wa IPC  Salim Asas alimshukuru  mbunge Kabati kwa kuendelea  kuwasaidia  wanahabari na jamii  nzima ya  jimbo la Iringa.

Alisema  kuwa  kinachofanywa na mbunge Kabati  kinapaswa  kuigwa na  wabunge  wengine  katika kuwasaidia  wanahabari ila  jamii inayowazunguka pia.

No comments: