Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Amos Makala akizungumza na wakazi wa manispaa ya Iringa wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Kajugusi akitoa ufafanuzi kuhusu Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kila mwaka nchini wakati wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma wakiangalia banda la Maonyesho la vijana wajasiriamali kutoka Zanzibar wanaoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiangalia gari lililotengenezwa kwa kutumia mbao na vifaa vya asili na mbunifu Keny Joseph kutoka kijiji cha Nyororo, Mufindi. Gari hilo ambalo limekua kivutio kikubwa katika maonyesho hayo analitumia katika shughuli zake za kila siku na lina uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 180 kwa saa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiingia ndani ya gari hilo.
Sehemu ya mbele ya gari hilo ambalo limewavutia vijana wengi wakati wa maonyesho ya wiki ya vijana mkoani Iringa kama inavyoonekana huku mbunifu wa gari hilo Bw. Keny Joseph (kushoto) akirekebisha baadhi ya vitu katika gari lake.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akipata maelezo kuhusu mifumo ya kompyuta katika banda la VETA mkoa wa Iringa wakati wa Maonyesho ya wiki ya Vijana kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Mlandege manispaa ya Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma (kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi wakitazama na kuonyesha kuvutiwa na baadhi ya bidhaa zilizokuwa katika banda la maonyesho la Vijana wa mkoa wa Dar es salaam.
Mkurugenzi Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Wanawake, Vijana na Wanawake kutoka Zanzibar Bw.Mohamed Salim Alli akifungua mdahalo wa Vijana wakati wa Wiki ya Vijana katika Ukumbi wa VETA mkoani Iringa.
Vijana wakishiriki mdahalo wa wazi wa Wiki ya Vijana , Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere , Mbio za Mwenge wa Uhuru na Fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Iringa leo katika ukumbi wa VETA Iringa.
Picha na Aron Msigwa- MAELEZO.
No comments:
Post a Comment