Monday, September 2, 2013

MKUTANO WA 10 WA MWAKA WA UMOJA WA KAMATI ZA BUNGE ZA HESABU ZA SERIKALI TOKA NCHI WANACHAMA WA SADC (SADCOPAC) WAFUNGULIWA NA PM MJINI ARUSHA LEO

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akipokelewa na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali Mhe. Ludovick Uttoh, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Zitto Kabwe na Mwenyekiti wa SADCOPAC Mhe. Sipho Makama kutoka Afrika Kusini alipokuwa akiwasili katika Ukumbi wa AICC Arusha kufungua Mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC kwaniaba ya Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya PAC Mhe. Zitto Kabwe akitoa salam za ukaribisho kwa wajumbe wote wa SADCOPAC.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akimkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC katika ukumbi wa AICC mjini Arusha.
Wajumbe wa mkutano wa SADCOPAC katika mkutano huo leo.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akihutubia wajumbe wa mkutano wa SADCOPAC kwaniaba ya Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu cha miaka kumi ya SADCOPAC mara baada ya kuhutubia wajumbe wa mkutano huo wa SADCOPAC kwaniaba ya Rais Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete leo.
Mgeni Rasmi akijibu maswali ya waandishi wa Habari.
Spika wa Bunge na Mgeni Rasmi wakifurahia kikundi cha ngoma mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa SADCOPAC.
CAG na Spika wa Bunge wakimsikiliza kwa makini Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda mara baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa SADCOPAC. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments: