Monday, September 2, 2013

MAANDAMANO YA WANAHABARI YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI YAFANYIKA LEO IRINGA

 Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali na  wadau  wa habari  mkoa  wa  Iringa  wakiwa katika  maandamano ya amani ya  kumuenzi  aliyekuwa mwenyekiti  wa klabu ya  waandishi  wa  habari  mkoa  wa Iringa (IPC) leo
 Maandamano  ya  wanahabari na  wadau  wa  habari yakipita  eneo la soko kuu la manispaa ya  Iringa
 katibu  wa IPC  Francis  Godwin  akiongoza  maandamano ya  wanahabari na  wadau huku akiwa  juu ya gari na picha ya marehemu Daudi Mwangosi
 Wanahabari  Iringa katika maandamano ya  kumuenzi  marehemu  Mwangosi  leo
 Maandamano ya  wanahabari  na  wadau  wa habari  mkoa wa Iringa ya  kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi  yakipita  eneo ya  uhindini 


 Wananchi  wakishuhudia maandamano  hayo  leo





 katibu  mtendaji  wa IPC  Francis  Godwin akitoa taarifa ya  kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi leo
 Katibu  wa  IPC Francis  Godwin mwenye pama akikabidhi maandamano ya  mwenyekiti  wa IPC Frank Leonard na  wadau  wengine  eneo la Maktaba ya  mkoa wa Iringa


 Katibu  wa  IPC  FrancisGodwin kushoto akikabidhi picha ya marehdemu Daudi Mwangosi kwa  mwenyekiti  wa IPC  Frank Leonard kulia,wanaoshuhudia ni mzee  Fulgence  Malangalila  na Majid Mjengwa


 Mwenyekiti wa  IPC Frank Leonard  kushoto akikabidhi  picha ya  Mwangosi kwa mwasisi  wa IPC mzee Fulgence Malangalila








Viongozi  wa  IPC kutoka  kulia Francis Godwin katibu  na Frank Leonard  mwenyekiti na mwakilishi  wa wananchi 

Na Francis Godwin
MAANDAMANO ya  wanahabari  mkoa  wa  Iringa  kwa  ajili ya  kumbukumbu  ya  mwaka  mmoja  ya  kifo  cha  aliyekuwa  mwenyekiti  wa klabu ya  waandishi  wa habari  mkoa  wa  Iringa (IPC) na mwandishi  wa Chanel  Ten Marehemu  Daudi Mwangosi  yatikisa mji  wa  Iringa leo
 
Maandamano  hayo ambayo  yameanza majira ya saa 4 asubuhi  katika  viwanja   vya  bustani ya  Manispaa ya  Iringa yamepita  kuzungu kakatika maeneo  mbali mbali ya  mji wa  Iringa kabla ya  kupokelewa na mwenyekiti  wa IPC  Frank Leonard katika  ukumbi wa maktaba ya  mkoa kwa mkutano wa  wadau  wa habari.
 
Maandamano  hayo yamepita  maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na  eneo la Uhindini , Mashine  tatu, Soko  kuu na stendi  kuu ya mabasi ya mikoani  wananchi  walilazimika  kusitisha  shughuli  zao kushuhudia maandamano  hayo ambayo yaliongozwa na  askari  wa  usalama barabarani.
Akizungumza  baada ya kupokea  maandamano  hayo ,mwenyekiti wa IPC Bw Leonard  alisema  kuwa  lengo la maandamano  hayo ni  kumkumbuka  Mwangosi pamoja na  kutazama  changamoto  mbali mbali ambazo  wanahabari  wamekuwa wakikabiliana.
Alisema  kuwa hakuna  mtanzania  asiyetambua  mchango  wa  Mwangosi  katika uhai wake  na  kuwa kutokana na mchango  wake  umoja  wa  vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania (UTPC) umeanzisha  tuzo maalum kwa wanahabari itakayopewa  jina la Daudi Mwangosi  na mshindi  atapewa kiasi cha  Tsh milioni 10.
Alisema  tuzo  hiyo  itakuwa  ikitolewa  kila mwaka  na UTPC na ili mwanahabari aweze  kushinda  tuzo hiyo ,lazima apitie katika misuko  suko katika  kazi  hiyo ,pia wale  watakaopigania  maslahi yao  na  fisa  nyingine  nyingi.
 Hivyo  aliwataka  wanahabari  wanachama  wa Vilabu  vya  wanahabari  na  wale wasio  wanachama  ambao  wanafanya kazi  Tanzania  kujitokeza   kuchangamkia tuzo hiyo.
Mbali   hilo  aliwataka  wanahabari  kuendelea  kuzingatia  maadili  yao  ya kazi hiyo  ili kuongeza imani kwa  watanzania .Alisema  kuwa wapo  wanahabari  watafanya  watazingatia  maadili  ya  uandishi  Taifa linaweza  kupiga  hatua  katika maendeleo.
Wakati  huo  huo IPC  imetoa  mikopo  ya  zaidi ya  Tsh 500,000 kwa  wanachama wake  ili kuwawezesha  kuboresha  zaidi  shughuli  zao kwa  kununua  vifaa vya kazi.
Marehemu   Mwangosi  aliuwawa  na  polisi septemba  2 mwaka 2012  katika kijiji  cha Nyololo  wilaya ya  Mufindi   wakati  wa  ufunguzi  wa  tawi la  Chadema kijiji  cha Nyololo.

No comments: