Wakati upepo mzuri wa kipindi cha joto kutoka bahari ya Hindi ukipuliza, uzinduzi wa mgahawa mjini Zanzibar, Six Degrees South, ulikuwa hauna mfano! Huku kukiwa na fataki za ndani, chupa za Moet zikifunguliwa kwa madaha usiku kucha mpaka mida ya usubuhi, uzinduzi wa Six Degrees South uliwaacha wengi mjini Zanzibar wamepigwa na butwa wakiwa hawana la kusema.
Huku Wanzibari wengi wakiwa wana hamu ya mgahawa kama huu, muundo wa mgahawa huu wa kisasa wenye ghorofa tatu umedhihirisha hadhi yake ya kuwa na eneo la nyama choma na baa ya mvinyo. Kuanzia ordha ya vyakula vya moto vya asubuhi mpaka mchanganyiko murua wa vyakula vya siku nzima na vitafunio vidogo vidogo, sehemu hii imeinua viwango vya biashara ya migahawa mjini Zanzibar na kuifikisha juu kabisa.
Six Degrees South ipo eneo la mji mkongwe na inawapa wageni utulivu wa hali ya juu ili kuwawezesha kupumzika na kujichanganya. Ukichanganya mazingira ya utulivu na na huduma ya bure ya mtandao wa internet, sehemu hii inamfaa mtu yoyote kupata kinywaji anachopendelea na vitafunwa. Mgahawa una vibaraza kwenye ghorofa tatu vyenye eneo kubwa kwa ajili ya wageni kutazama jua likizima kwenye mandhari ya Bahari ya Hindi.
Vyakula kutoka mataifa mbalimbali pia vitapikana kwa ya wateja wenye ladha na uwezo tofauti. Orodha ya chakula iliyoandaliwa na Mpishi Mkuu kutoka Afrika Kusini, Louise Serfontein, inatoa fursa kwa watu kutoka bara na visiwani kufuruhia chakula. Six Degrees South inajisifia kwa kuwa na viwango vya hali ya juu ya utoaji huduma wakati wakiwaridhisha wateja kwa chakula na mandhari nzuri.
Huku wakiwa na orodha ya mivinyo zaidi ya 80 ambayo mteja anaweza kunywa kwa glasi au chupa, Six Degrees South inatoa fursa nzuri ya kunywa, kula na kufanya matembezi wakati mwezi ukiangaza kwenye bahari.
Sehemu yenye kutoa ukarimu wa hali ya juu, Six Degrees South ni sehemu ambayo kila mtu anatakiwa kutembelea.
-
No comments:
Post a Comment