Sunday, September 29, 2013

GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHINGTON, DC YAFANA


Wageni wakiwa kwenye foleni ya kupata chai ya Tanzania na vitafunio kama vile Vitumbua, maandazi na kadhalika na wengine wakijionea nguo na vitabu vya kiswahili.
 Wageni wakiendeea kujionea, kula na kusikiliza vivutio vingine vilivyopo Tanzania kwa Walimu wa darasa la kiswahili DMV wakijaribu kuwaelezea uzuri wa Tanzania na vivutio vyake.
 Walimu wa darasa la kiswahili wakiwaelezea wageni waliotembelea banda la Tanzania upikaji wa vitafunio walivyoleta.
 Mmoja ya mgeni aliyetokea Virginia akipata chai na kitumbua huku akisifia utamu wake.
 Walimu wa darasa la kiswahili katika picha ya pamoja.
 Watoto wa darasa la kiswahili wakiimba baadhi ya nyimbo za Tanzania
 Mgeni akipata maelekezo ya vitabu vya kiswahili huku akiwa na kibakuli cha maandazi.
 Banda la Tanzania katika picha ya pamoja.
 Mzee Safari (kulia) akimuelezea moja na mgeni kuhusu kitabu chake cha "Nyayo za Obama" alichatunga kwa Kiswahili

No comments: