Friday, August 30, 2013

UJUMBE WA ZANZIBAR WAKUTANA NA WAZIRI MKUU NA KAMPUNI YA SAKURA NCHINI UHOLANZI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark Rutte,alipofika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara na Ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark Rutte,alipofika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara na Ujumbe aliofuatana nao,(kushoto) Waziri wa Ardhi,Maji,Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifuatana na Mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Serikali ya Uholanzi Mark Rutte,baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ya Waziri huyo Nchini The Hague Uholanzi akiwa katika ziara ya Kiserikali na Ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Bibi Regine Aalders,kutoka Wizara ya Afya nchini Uholanzi,wakati alipotembelea katika Ofisi ya Kampuni ya Sakura Finatek jana,ambayo inatengeneza Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,nje ya Mji wa The Hague Nchini Uholanzi akiwa katika ziara ya Kiserikali.
Bibi Regine Aalders,kutoka Wizara ya Afya nchini Uholanzi,alipokuwa akiwasilisha mada wakati wa mkutano wa kampuni ya Sekura na Makampuni mengine wakati walipokutana na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar nchini humo kwa ziara ya Kiserikali ambapo ziara hiyo itamalizika kesho.
Baadhi mya Viongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na wenyeji wao Viongozi wa kampuni ya Sakura Finetek Europe,inayojishuhulisha na Utengenezaji wa Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,iliyopo nje ya Mji wa The Hague Nchini Uholanzi wakiwa mkutano wa kufikia kuongeza kasi ya kutoa huduma bora za Kiafya katika ziara ya Kiserikali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akitoa hutuba yake wakati wa mkutano na Kampuni ya Sakura Finetek Europe, inatengeneza Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa Binadamu,wakati alipotembelea katika Ofisi ya Kampuni hiyo jana,iliyopo nje ya Mji wa The Hague Nchini Uholanzi,Rais akiwa katika ziara ya Kiserikali.
Baadhi ya Viongozi na Maafisa wa Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika mkutano wa Ushirikiano na kampuni ya Sakura Finetek Europe,katika hatua za makusudi katika kuongeza kasi ya utoaji wa Huduma za Kiafya,walipokuwa katika ziaraya Kiserikali nchini Uholanzi.
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwa katika mkutano wa Ushirikiano na kampuni ya Sakura Finetek Europe,katika hatua za makusudi katika kuongeza kasi ya utoaji wa Huduma za Kiafya,walipokuwa katika ziara ya Kiserikali nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mtaaalamu wa matumizi ya Vifaa vya maabara Robert Heijmen,alipotembelea mashine mbali mbali za uchunguzi wakati wa mkutano na Kampuni ya Sakura Finetek Europe, inayotengeneza Vifaa vya maabara vya Uchunguzi wa maradhi ya Binadamu, jana akiwa katika ziara ya kiserikali nchini uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea Cheki kutoka kwa Rais,pia Meneja Mkuu wa kamapuni ya Sakura Finetek Europe, Chris Koeman,kwa ajili ya Uchunguzi wa Maradhi ya binadamu katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,wakati wa mkutano wa ushiriano katika kukuza huduma na kampuni hiyo,na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,katika ziara Nchini Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Kamapuni ya Sakura Finetek ,baada ya mkutano uliofanyika jana baina ya kampuni na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ukiwa katika ziara Nchini Uholanzi. .[ Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]

No comments: