Tuesday, August 13, 2013

SHIRIKA LA UNESCO LAKUSUDIA KUVIJENGEA UWEZO VYOMBO VYA HABARI VYA JAMII KUKUZA AMANI NA DEMOKRASIA NCHINI

IMG_2158
Makao Makuu ya kituo cha habari na mawasiliano cha Redio ya jamii Sengerema Fm mkoani Mwanza kunakofanyika warsha ya wiki moja kwa redio za jamii nchini kwa ajili ya kuziandaa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
IMG_1954
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Radio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye akiwakaribisha na kuwatambulisha wawezeshaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa Wakurugenzi na Mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya wiki moja iliyoandaliwa na UNESCO kupitia mradi wa DEP kwa ajili ya kuwaanda kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
IMG_1906
Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin akizungumza na mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania nchini katika warsha ya wiki moja juu ya matayarisho ya mradi wa kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia kwa jamii kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.
IMG_1964
Mshauri wa Redio Jamii kutoka UNESCO Mama Rose Haji Mwalimu akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoani Mwanza. Wa pili kushoto ni Meneja wa Mradi wa DEP kutoka UNESCO Courtney Ivins, Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam ambaye pia ni Mtafiti kutoka ECOM Research Dr. Ambrose Kessy.
IMG_1943
Meneja wa Redio Sibuka Fm Maswa Bi. Bhoke Okachu akiwasilisha maoni wakati wa kujadili mradi wa DEP kwenye warsha ya wiki moja inayoendelea wilayani Sengerema mkoani Mwanza.
IMG_1909
Picha juu na chini ni Sehemu ya washiriki ambao ni Mameneja na Wakurugenzi wa redio za jamii 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaohudhuria warsha hiyo.
IMG_1971
IMG_1917
Meneja wa Kyela Fm Lucas Kulwa akichangia maoni yake wakati wa warsha hiyo.

Na. Mwandishi wetu

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni(UNESCO) limesema kwamba linakusudia kuvijengea uwezo vyombo vya habari vya jamii ili kuviwezesha vyombo hivyo kuandaa vipindi vya elimu kuhubiri mijadala ya Amani na Demokrasia (DEP) kuelekea uchaguzi wa mwaka 2015.

Afisa Mipango Taifa wa Kitengo cha Mawasiliano na Habari UNESCO Yusuph Al Amin amesema UNESCO, UNDP, UN WOMEN, wamekusudia kufanya hivyo kwa dhamira ya kuvitayarisha vyombo hivyo mapema baada yakuona changamoto nyingi zilizojitokeza katika uchaguzi wa mwaka 2010, ambapo elimu ya kutosha haikuwafikia wananchi waliowengi.

Yusuph ameyasema hayo katika kituo cha habari na mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza, wakati akiwasilisha mada ya amani na demokrasia kwa mameneja , wakurgenzi wa redio za jamii Tanzania, wasimamizi wa redio za halmashauri na mazingira Tanzania bara katika warsha ya wiki moja juu ya matayarisho ya redio hizo katika uchaguzi ujao.

Uhamasishaji wa elimu ya wapiga kura, usawa wa kijinsia katika kuhamasisha kinamama kushiriki katika uchaguzi kwenye kujiandikisha, kupiga kura nakujitokeza kugombania nafasi mbalimbali za uongozi na kutoyafikia makundi maalum ipasavyo licha ya mafanikio makubwa yaliyofikiwa ukilinganisha na muda mchache wa elimu uliotumioka kabla ya uchaguzi ni mambo muhimu yaliyohamasisha elimu hio kutolewa mapema Yusuph alisema.

Amebainisha kuwa katika kuhakikisha ufanisi mkubwa unafikiwa katika uchaguzi ujao, wameongeza redio shiriki kutoka 12 hadi 25, huku manufaa zaidi yakielekea visiwani ambapo redio ya jamii Tumbatu na redio jamii kusini Pemba, zitaanzishwa na redio Uvinza mkoani Kigoma ambazo kwa pamoja zitapewa mafunzo yakutosha ikiwa ni pamoja na viongozi wa bodi, watu mashuhuri, viongozi wa halmashauri na viongozi wa dini.

Al Amin amesema kutokana na uzoefu, chaguzi zilizopita katika nchi jirani na matokeo yake, uchaguzi ujao huenda kukawa na changamoto nyingi, hivyo ni vyema kuhamasisha majadiliano ya amani yatiliwe mkazo na kuboresha mawasiliano na taasisi husika ambapo watendaji 250 wa habari watapewa mafunzo na watanzania milioni nane watafikiwa kupata taarifa kupitia redio za jamii.

Amesisitiza kuwa kazi ya kuhubiri amani na demokrasia inahitaji kuvumiliana kutokana na changamoto zilizopo na kuwa vyombo vya habari, ni vyema kujua miiko na usawa katika utendaji hasa katika kuandika na kutangaza taarifa zinazohusu uchaguzi, huku akivilaumu vyombo vya habari kwa kuhubiri uajibikaji kwa wengine, bali wao wamekuwa na mapungufu mengi na hawanabudi kufanya marekebisho mapema.

Amesema vyombo vya habari vya jamii, huu ni wakati muafaka wa kufanya mabadiliko katika watendaji wake kutokana na idadi ndogo ya watangazaji na waandishi na maripota wanawake kupungua siku hadi siku, kuboresha vipindi na kufahamu kuwa utamaduni wa watanzania ni amani na vyema kudumisha utamaduni huo kuanzia vyombo vya habari vya jamii.

No comments: