Meneja wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila akizungumza juu ya umuhimu wa mtandao huo wakati wa kutoa msaada kwa watoto yatima kituo cha Amani Nsagala Uyole.
Baadhi ya watoto katika kituo cha Kulelea yatima cha Aman Nsagala uyole wakimsikiliza kwa makini Meneja wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila
Mmoja ya wananchi waliokiuja kushuhudia kutolewa kwa Msaada huo , akiuliza swali juu ya Tovuti hiyo.
Baadhi ya watoto katika kituo cha watoto yatima cha Aman Nsagala wakiimba Nyimbo kabla ya kukabidhiwa msaada huo.
Meneja wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila kushoto akikabidhi msaada wenye thamani ya Tsh 1,500,000 katika kituo kituo cha kulelea watoto yatima cha Amani
Hili ni eneo ambalo watoto hawa hukutania na kujifunza mambo kadha wa kadha
Msimamizi Msaidizi wa Kituo hicho kilicho chini ya Idara ya Wanawake ya Kanisa la Moraviani, Isabela Haonga akitoa neno la Shukurani kwa kampuni ya LAJANN E-SYSTEM ENTERPRISES kwa msaada uliotolewa kwa watoto yatima
Meneja wa Kampuni inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao, Nzowa Wawila akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Aman Nsagala Uyole.
********
JAMII imetakiwa kuisaidia Serikali katika kuifichua na kuziba mianya inayosababisha Watoto wa mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu kuzidiu kuongezeka licha ya Asasi nyingi kujitokeza kuwahudumia.
Mwito huo ulitolewa wa na Katibu Mkuu wa Jimbo la Kusini Magharibi la Kanisa la Moraviani Tanzania, Mchungaji Willy Mwasile, wakati akipokea msaada kutoka kwa kampuni ya LAJANN E- System Enteprises ya Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya kituo cha kulelea watoto Yatima cha Aman Nsalaga kilichopo Uyole Jijii Mbeya.
Mchungaji Mwasile alisema ni vema utafiti ukafanyika ili kubaini chanzo cha ongezeko la Yatima mitaani ili liweze kudhibitiwa na kuondolewa kabisa kwa kudhibiti ndoa zisizo halali kwa wale wanaobeba mimba kiholela na kutokuwa na uwezo wa kulea.
Akitoa msaada huo Meneja wa Kampuni hiyo inayojishughulisha na kurusha matangazo yanayohusu ligi ya mpira wa miguu ya Tanzania kupitia mtandao huu www.ligikuu.co.tz , Nzowa Wawila, alisema kutokana na kukaribia kufunguliwa kwqa pazia la Ligi kuu wameona ni vema wakatoa msaada kwa jamii ili kutambua umuhimu wao.
Alisema kampuni yao inayofadhiliwa na Benki ya Banc ABC imeona siyo vizuri misaada yote ikaishia Dar Es Salaam pekee ili hali kunawahitaji wengi mikoani na ndiyo maana wakafika katika kituo cha Amani Nsalaga na kutoa msaada.
Alivitaja vitu vilivyotolewa kuwa na thamani ya Shilingi Milioni Moja na Nusu( 1,500,000/=) zikiwa ni kwa ajili ya Mchele debe 10, maharage debe 5, Sukari katoni 2 sabuni, kalamu chumvi na vifaa vya shule.
Aliongeza kuwa kampuni yao inahusika zaidi na michezo na kwamba katika zawadi ambazo walipaswa kuzitoa ilikuwa ni vifaa vya michezo lakii wameshindwa kufanya hivyo kutokana na mahitaji ya kituo kwamba watoto wanatakiwa kula na kusoma hivyo vifaa vya michezo vitatolewa hapo baadaye.
Kwa upande wake Msimamizi Msaidizi wa Kituo hicho kilicho chini ya Idara ya Wanawake ya Kanisa la Moraviani, Isabela Haonga, akishgukuru kwqa niaba ya watoto alisema msaada huo utasaidia kuboresha maisha ya watoto kutokana na wengi wao kulelewa katika mazingira magumu.
Alisema kituo hicho kinahudumia zaidi ya watoto 200 kwa kuwatafutia sare za shule, ada na mahitaji yote ya shule, kuwajenga kisaikolojia, kuwakatia bima za Afya pamoja na chakula hali inayosababisha Kitengo hicho kushindwa kumudu gharama zote na kuomba msaada kwa wasamaria wema wengine kujitokeza kutoa msaada.
No comments:
Post a Comment