Tuesday, August 27, 2013

Katibu Mkuu na Naibu wake wapokewa kwa Shangwe Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga mwenye nguo nyekundu akipokea zawadi ya maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo Bibi Mwanakombo Jumaa katika hafla ya kupokea uongozi mpya leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga mwenye nguo nyekundu akipokea zawadi ya maua kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Magazeti la Serikali (TSN) wakati wa hafla ya mapokezi ya kumkaribisha Katibu Mkuu huyo leo jijini Dar es Salaam 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifurahi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambao wameteuliwa hivi karibuni.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga kulia akikaribishwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bwana Seth Kamuhanda.Tukio hili limefanyika leo jijini Dar es Salaam baada ya makabidhiano rasmi ya ofisi 
 Kutoka kushoto ni aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seth Kamuhanda akikabidhiwa zawadi ya picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea viongozi wapya na kukabidhi ofisi.Kulia ni Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi Sihaba Nkinga mwenye nguo nyekundu akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara hiyo Profesa Hermas Mwansoko leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kupokea viongozi wapya na kukabidhiwa ofisi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni, na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel kushoto akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko lleo jijini Dar es Salaam katika hafla ya mapokezi yao iliyoandaliwa na wafanyakazi wa Wizara hiyo.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bwana Seth Kamuhanda (katikati) akiteta jambo na Katibu Mkuu mpya wa wizara hiyo Bibi Sihaba Nkinga (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia)
Wafanyakazi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakifurahi wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambao wameteuliwa hivi karibuni.

No comments: