Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP. Mohammed R. Mpinga akiongea na kuwaasa madereva wa Bodaboda wakati wa kufunga mafunzo hayo. Kushoto kwa Kamanda ni Rais wa AAT Mr Nizan Jivan, CEO wa AAT Mr Yusuf Aghor na Mweka hazina wa AAT Mr Pepe.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed Mpinga akikabidhi cheti kwa mhitimu Mwanamke aliyehitimu mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani yaliyotolewa kwa madereva wa Bodaboda Dsm na Kikosi cha Usalama Barbarani kwa kushirikiana na AAT (Automobile Association of Tanzania) kwa ufadhili wa chama cha mashindano ya Magari Duniani (FIA) wakati ufugaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika Gongolamboto 10/07/2013. Anayeangalia ni Rais wa AAT Mr Nizan Jivan
Mr Nizan Jivan Rais wa Automobile Association of Tanzania (AAT) akiongea na madereva wa Bodaboda wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika Gongolamboto – Dar es salaam 10/07/2013. Kulia ni Mr Yusuf Aghor CEO wa AAT na kushoto ni ASP Swai wa Makao Makuu ya Traffic Dsm.
Mr Nizan Jivan Rais wa Automobile Association of Tanzania (AAT) akipokea zawadi maalum kutoka kwa wahitimu wa Mafunzo ya dereva wa BODABODA mkoani Dar es Salaam kama shukrani yao ya pekee kwa kudhamini mafunzo haya bure kwa madereva wa Bodaboda, ufugaji wa mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda ulifanyika Gongolamboto Dsm tarehe 10/07/2013.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed R. Mpinga (kushoto) akikabidhiwa Tuzo maalum ya ushiriki wake katika kusimamia mafunzo ya Bodaboda mkoa wa Dar es Salaam. Tuzo hiyo alikabidhiwa na Rais wa Automobile Association of Tanzania (AAT) Mr Nizani Jivan wakati wa ufungaji wa mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda tarehe 10/07/2013 Gongolamboto – Dar es salaam.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed Mpinga akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Automobile Association of Tanzania (AAT) na wadau mbalimbali waliohudhuria katika ufugaji wa mafunzo ya elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda, tarehe 10/07/2013 Gongolamboto - Dsm.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani – DCP Mohammed R. Mpinga akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda katika ufugaji wa mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 10/07/2013 Gongolamboto – Dsm.
Madereva Bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam wakipokea kiapo chao cha utii kuashiria kuwa mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani waliyoyapata darasani sasa watayafanya kwa vitendo wawapo katika kazi zao za usafirishaji wa abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam. Kiapo hiki kilifanyika mbele ya Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani DCP Mpinga wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo kwa madereva wa Bodaboda Gongolamboto 10/07/2013.
Sehemu ya Madereva Bodaboda wa mkoa wa Dar es Salaam wakimsikiliza Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani pichani hayupo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya Elimu ya Usalama Barabarani kwa madereva wa Bodaboda. Ufugaji wa mafunzo hayo ulifanyika Gongolamboto tarehe 10/07/2013.
No comments:
Post a Comment