Mtoa mada iliyohusu Maadili
kazini,Bwa.Alex Senzota kutoka Idara ya Usalama Kazini (GSO),akifafanua zaidi
kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi husika,mapema leo kwenye Kongamano la Tatu la Makatibu
Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) uliofanyika ndani
ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Mwenyekiti
wa Chama chama cha Makatibu Muhtasi Nchini Uganda (NASAP),Bi Edith Kutesa
Giita akifafanua jambo kuhusiana na mada mojawapo ya iliyohusu Ni namna gani
unaweza kuwa Katibu Muhtasi unaekwenda na wakati/wa kisasa,mapema leo
kwenye Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal
Secretaries Association - TAPSEA) lililofanyika ndani ya ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa chama cha Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA),Bi Pili Mpenda akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi likiendelea ndani ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha,kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama chama cha Makatibu Muhtasi Nchini Uganda (NASAP),Bi Edith Kutesa Giita.
Baadhi washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazojadiliwa kwenye kongamano hilo lililofanyika dani ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Mmoja wa wachangia mada kutoka chuo cha Sokoine,Bi Teddy Salum akizungumza kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi,wakati Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) likiendelea ndani ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Mmoja wa wachangia mada kutoka chuo Kikuu cha Dar- Es Salaam (UDSM),akifafanua jambo kuhusiana na mada iliyohusu Maadili kazini na namna ya kutunza/kuepuka uvujaji wa siri za ofisi,wakati Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) likiendelea ndani ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Sehemu ya washiriki wa Kongamano la Tatu la Makatibu Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zinazojadiliwa kwenye kongamano hilo lililofanyika dani ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Arusha (AICC), Jijini Arusha.
============= ======= ===========
IMEELEZWA VIONGOZI NDIYO CHANZO CHA UVUJAJI WA SIRI MAKAZINI NA SI MASEKRETARI.
Suala la uvujaji
kwa siri kwa baadhi ya sehemu kubwa ya maofisi makazini,imeelezwa kuwa chanzo
kikubwa ni viongozi na si makatibu Muhtasi kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakieleza.
Hayo yameelezwa leo kwenye siku ya pili ya Kongamano la Tatu la Makatibu
Muhtasi (Tanzania Personal Secretaries Association - TAPSEA) uliofanyika ndani
ya ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
Arusha (AICC), Jijini Arusha.
Akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali, mtoa mada iliyohusu Maadili
kazini,Bwa.Alex Senzota kutoka Idara ya Usalama Kazini (GSO),alipata wakati
mgumu wa kujibu maswali kutoka kwa washiriki wa kongamano hilo kuhusiana na
mada hiyo iliyozua mjadala mkubwa ukumbini humo.
Mmoja wa washiriki katika kongamano
hilo aliyejitambulisha kwa jina la Teddy Salum kutoka chuo cha Sokoine,alieleza
kuwa tatizo kubwa la uvujaji siri kwa asilimia kubwa linatokana na Viongozi wenyewe
kutokana na itikadi zao za kisiasa ama ya kutaka umaarufu.
Aidha Mshiriki Mwingine alibainisha kuwa tatizo hilo la uvujaji siri maofisini
linatokana na baadhi ya viongozi a.k.a MABOSS
kutozingatia/kupuuza ama kutokuwa na maadili ya kazi katika kuhakikisha siri za
ofisi husika zinatunzwa ipasavyo,ili kulinda usalama wa ofisi husika.
Mtoa Mada wa Maadili kazini,Bwa.Alex Senzota alifafanua kuwa kutokana na
tatizo hilo kubainika kuwa kubwa katika kongamano hilo,kuna haja ya Serikali
kuangalia mfumo mzima wa kuhakikisha maadili ya kazi yanazingatiwa katika Nyanja
zote zote,hasa kwa watumishi wa umma.
Kongamano
hilo la siku mbili, limehudhuriwa na Makatibu Muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka
mikoa yote nchini, na baadhi ya wawezeshaji kutoka Kenya, Uganda na Rwanda.
No comments:
Post a Comment