Tuesday, March 26, 2013

UMOJA WA MATAIFA WAKUMBUKA UTUMWA NA BIASHARA YA UTUMWA

 BANGO  lilombeba ujumba wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya  kumbukumbu ya  utumwa na biashara ya utumwa, maadhimisho ambayo yalifikie kilele Marchi 25 hapa  Umoja wa Mataifa.
Biashara ya utumwa haikufanyika kupitia bahari ya Atlantik peke yake bali hata Bahari ya Hindi kwa watumwa waliotoka Afrika ya Mashariki, Balozi za Tanzania na Kenya katika Umoja wa Mataifa, zilifanya onesho la Khanga zilizobeba ujumbe mbalimbali, kama sehemu ya kuenzi utamaduni mwa mwafrika na wakati huo huo kukitangaza kiswahili, washiriki wa tamasha la utamaduni ambalo lilikukwenda samabamba na vyakula vya asili ya afrika walifurahia sana tafsri ya kila ujumbe uliokuwa katika khanga hizo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza wakati wa maadhimisho hayo, ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza Jumuiya ya Kimataifa kuendelea kupambana na utumwa unaoendelea hivi sasa kila pembe ya dunia.
wanamuziki hawa walisindikiza mwanamziki mwigine kutoka Afrika ya Magharibi, Benyoro ambay naye alikuwa kivutio kikubwa.
Somi Mwanamziki wa Kizazi kipya wa Muziki wa Jazi, kutoka Afrika ya Mashariki naye aliwapagaisha washiriki wa tamasha la muziki kwa vibao vyake murua vilivyokuwa na radha ya muziki wa Jazi kwa kuchanganya na midundo ya kibantu ambayo mwenyewe anaita " New African Jazz" Somi alitambuliwa kama Baba yake ni Muganda na Mama yake Mnyarwanda.
Kikundi cha Utamduni kutoka nchini Cameroon wakitumbuiza wakati wa Tamasha maalum la Muziki kuadhimisha kumbukumbu ya waathirika wa utumwa.
wanamuziki hawa waliokuwa pamoja na Steel Pulse wakicharaza magitaa yao kwa uhodari mkubwa pali kuwa hapatoshi.
Steel Pulse mwanamuziki wa kimataifa wa muziki wa Rock ambaye amekuwa akitumia kipaji chake kuelimisha na kuhamasisha kuhusu ukatili anaotendewa mtu mweusi, Bw. Steel Pulse alikuwa kati ya wanamuziki waliotumbuiza katika tamasha maalum la kuwaenzi waathirika wa utumwa na biashara ya utumwa.
Mwanamuzi mwingine maarufu kwa kulicharaza gitaa na ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa UNESCO katika mradi wa kutafiti njia za Biashara ya Utumwa akiimbia kwa hisia kali wakati wa Tamasha la Muziki, Marcus Miller amewahi kushinda mara mbili Tuzo ya Grammy katika midundo ya American Jazz.
Professa Ali Mazrui, Mwanazuoni maarufu akisaidiwa kuketi kabla ya kuzungumza katika siku hii ya maadhimisho ya kumbukumbu ya utumwa na biashara ya utumwa .
hii ni Nakala Halisi ya Tangazo la Ukombozi wa Watumwa ( Emancipation Proclamation) iliyotiwa sahihi mwaka 1864 na Rais Abraham Lincoln na aliyekuwa Waziri wake wa Mambo ya Nje wakati huo, Bw. William H. Seward. Nakala hii ambayo ilioneshwa pamoja na maonesho mengine yaliyohusu utumwa na biashara ya utumwa ni kati ya nakala 48 ambazo Rais Lincoln alizisaini, na zikauzwa kwa dola kumi kila moja kati ya juni 7 hadi 29, 1864 huko Philadelphia kwa lengo la kupata fedha za kuwasaidia maveterani wa vita. inasemekana ni kati ya nakala hizo 48 ni 26 tu ndiyo bado zipo moja ikiwa ni hii ambayo ilipatikana kwa hisani ya Bw. Lawrance Benson.
hawa pia wanatoka Cameroon wakiburudisha.
Professa Mazrui akizungumza ambapo pamoja na mambo mengine alielezea histotia ya utumwa na biashara ya utumwa pamoja na harakati mbalimbali zilizopelekea kukomeshwa kwa biashara hiyo. pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa kuendelea kuwaenzi waathirika wa ukatili huo, alitaka pia kuenzi yale mema ambayo baadhi yake ni matokeo ya historia hiyo ya Utumwa, Professa Mazrui alikuwa mzungumzaji mkuu katika maadhimisho haya ambayo hufanyika Machi 25 ya kila mwaka.

No comments: