Sunday, March 3, 2013

MAZOEZI YA MBIO ZA POLE POLE ZA BIAFRA SPORTS CLUB ZAFANA LEO


Kama ilivyo ada, baada ya kuhairishwa ka safari ya kwenda Kunduchi wanamichezo toka vilabu vya Namanga na Biafra waliamua kufanya mazoezi pamoja kwa kuanzia Namanga jijini Dar es salaam  na kuishia Biafra. Mbio hizo zilipita katika bara ya Ubalozi (USA), Mwai Kibaki, Migombani, Mission Mikocheni, New Bagamoyo, , Mwinjuma, Hospitali ya Mwananyamala, Dunga, Kawawa na kuishia 90 Degrees Pub ambapo ni Makao makuu ya klabu y Biafra. 
Jogging barabara ya ubalozi (USA)


Katibu Mkuu wa Biafra Kaka Poli akiongoza jahazi...ingawa rejeta inaonekana kufuka moshi tehe tehe tehe...







Mara baada ya kumaliza jogging wanamichezo waliendelea na mazoezi ya aerobics yaliyokuwa yakiongozwa na mwanabiafra Khamis Suleiman (mwenye fulana nyekundu pichani chini).
 


Wanamichezo wote baada ya kutula walikaribishwa na Katibu Mkuu wa Biafra na baada ya pongezi za kushiriki na kumaliza mbio kwa wanamichezo wotw, taarifa mbalimbali zilitolewa ikiwemo ya  maendeleo ya mchakato wa kuanzisha Shirikisho la Jogging Manispaa ya Kinondoni pamoja na hatua zilizochukuliwa katika kuhuisha Chama cha Mchezo wa Jogging Kinondoni.
Katibu wa Biafra akiwakaribisha wanamichezo

Mapumziko

Kutoka kushoto; Mary, Kaka Poli, na Bebee

 Safari yetu ya Kunduchi itafanyika jumapili ya tarehe 10 Machi, 2013. Karibuni wadau wote!!!
MAZOEZI NI AFYA ACHA KUJIACHIA!!!

No comments: