Wednesday, February 27, 2013

  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo
  Akiwa amevalia vazi la asili la akina mama wa kabila la Wafipa, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anashiriki kucheza ngoma ya kabila hilo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga
  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha akinamama cha Upendo kilichoko katika makao makuu ya wilaya ya Kalambo katika mji wa Matai tarehe 26.2.2013. Akinamama hao wapatao kumi hujishughulisha na kazi ya kukamua mafuta ya alizeti. 

 Mjumbe wa NEC ya Chama Cha Mapinduzi Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha Mafundi seremala kiitwacho Kazimoto kilichoko kaika mji wa Matai wilayani Kalambo
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Matai waliofurika katika eneo la soko jipya mjini hapo ili kushiriki katika sherehe ya kukabidhi pikipiki kumi kwa ajili ya watendaji wa vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi

 Mke wa rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa baadhi ya vikundi vilivyoshiriki katika shughuli ya kukabidhi pikipiki kwenye vituo vya afya vya mikoa ya Rukwa na Katavi zilizofanyika huko Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa mji wa Matai waliohudhuria sherehe ya kukabidhi pikipiki kwa ajili ya vituo vya afya katika mikoa ya Rukwa na Katavi iliyofanyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa












No comments: