Thursday, February 21, 2013

kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara

 Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Mh. Wilman Kapenjama Ndile (kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara leo,tayari kwa ufunguzi wa Kongamano hilo ambalo ni la siku mbili.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid (kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia (katikati) na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro wakifatilia Kongamano hilo.
Mwenyekiti wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),John Bwire akitoa utambuliwa wa Wanahabari waliohudhulia kongamano hilo toka sehemu mbali mbali hapa nchini,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Emmanuel Humba akitoa taarifa fupi ya Mfuko wa Bima ya Afya kutokana tafiti mbali mbali zilizofanywa na baadhi ya Wanahabari katika Halmashauri 26 hapa nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara mjini,Mh. Wilman Kapenjama Ndile akisalimia.
Wakijajiliana jambo.
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri wa vyombo vya Habari hapa nchini,Nevile Meena akizungumza machache wakati wa Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,linaloendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Raphael Mwamotto akitoa muongozo na utambulisho kwa baadhi ya viongozi kutoka sehemu mbali mbali wanaohudhulia Kongamano hilo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Eugin Mikongoti akiwasilisha mada yake kwenye Kongamano la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Wadau wakifatilia Mada zinazotolewa kwenye Kongamano hilo.
Wadau.
Mkuu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Athuman Rehani akiweka sawa mambo kabla ya kuwasilisha mada yake.
Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wadau wa NHIF wakiwajibika.
Wakuu wa Wilaya za Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Baadhi ya Wanahabari kutoka Vyombo mbali mbali vya Habari wakifatilia kwa makini Kongamano hilo la nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Picha na Othman Michuzi.

No comments: