Friday, January 11, 2013

MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA PILI, 2012

1.0               UTANGULIZI
Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili ulifanyika nchini kote kuanzia tarehe 05/11/2012 na kumalizika tarehe 16/11/2012. Mwaka 2012 kulikuwa na jumla ya vituo 4,304 vilivyosajili watahiniwa, ikiwa ni ongezeko la vituo 117(2.79 %) ikilinganishwa na ile ya mwaka 2011.
2.0              WATAHINIWA WALIOSAJILIWA, WALIOFANYA NA WASIOFANYA MTIHANI
2.1                Idadi ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 430,327, kati yao wasichana walikuwa 205,476 na wavulana 224,851. Idadi hii ni upungufu wa watahiniwa 36,240 (7.76%) ikilinganishwa na mwaka 2011 ambapo walikuwa 466,567.
2.2               Watahiniwa 386,271 sawa na asilimia 89.76 ya waliosajiliwa, walifanya mtihani wakiwemo wasichana 187,244 na wavulana 199,027.
2.3               Watahiniwa 44,056 sawa na asilimia 10.24 hawakufanya mtihani, kati yao wasichana ni 18,231 na wavulana 25,825. Mwaka 2011 watahiniwa 47,527(10.19%) hawakufanya mtihani. Sababu za watahiniwa kutofanya mtihani ni pamoja na utoro, kuugua,  kudaiwa ada, kufukuzwa shule, mimba na vifo.
3.0              UFAULU WA WATAHINIWA
3.1                Watahiniwa waliofaulu ni 249,325 (64.55 %) kati yao, wasichana ni 113,213 na wavulana 136,112.  Kiwango cha ufaulu kimepanda kwa asilimia 19.15 kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011. Watahiniwa waliofaulu kwa kiwango cha A, B, na C walikuwa 127,981 (33.13%) na waliofaulu kwa kiwango cha D ni 121,344 (31.42%). Alama ya juu ya ufaulu ni 92%
3.2               Wastani wa ufaulu kwa masomo ni 38%, wastani huu umepanda kwa asilimia 7 ukilinganishwa na  mwaka 2011 ambapo ulikuwa 31%.
3.3               Watahiniwa 136,923 (35.45 %) hawakufaulu mtihani, wakiwemo wasichana 74,020 na wavulana 62,903. Watahiniwa hawa watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Aidha, mwaka 2011 watahiniwa 228,759 (54.59%) hawakufaulu mtihani.
3.4               Watahiniwa 23 matokeo yao yamefutwa kutokana na tuhuma za udanganyifu. Watahiniwa hawa wanatoka katika shule zifuatazo;
Na
Jina la Shule
Kanda
Idadi ya watahiniwa
1.
Kiyongwire
Mashariki
2
2.
Nyashishi
Ziwa
4
3.
Thaqaafar
Ziwa
3
4.
Paroma
Ziwa
2
5.
Murangi
Ziwa
1
6.
Bukene
Magharibi
7
7.
Kili
Magharibi
1
8.
Binza
Magharibi
1
9.
Kizumbi
Magharibi
1
10.
Kolandoto
Magharibi
1

Watahiniwa hawa nao watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013.
4.0              UFAULU KWA SHULE
4.1               Shule Zilizoshika Nafasi Kumi za Mwanzo
4.1.1          Shule za Serikali
NA.
SHULE
KANDA
1.
MZUMBE
MASHARIKI
2.
TABORA WAVULANA
MAGHARIBI
3.
ILBORU
KASKAZINI MAGHARIBI
4.
KIBAHA
MASHARIKI
5.
IYUNGA
NYANDA ZA JUU
6.
MSALATO
KATI
7.
MALANGALI
NYANDA ZA JUU KUSINI
8.
IFUNDA  UFUNDI
NYANDA ZA JUU KUSINI
9.
SAMORA MACHEL
NYANDA ZA JUU
10.
KILAKALA
MASHARIKI
4.1.2         Shule Zisizo za Serikali
NA.
SHULE
KANDA
1.
KAIZIREGE
ZIWA MAGHARIBI
2.
MARIAN WAVULANA
MASHARIKI
3.
ST. FRANCIS
NYANDA ZA JUU
4.
DONBOSCO
NYANDA ZA JUU KUSINI
5.
BETHEL SABS
NYANDA ZA JUU KUSINI
6.
MARIAN WASICHANA
MASHARIKI
7.
DON BOSCO (MOSHI)
KASKAZINI  MASHARIKI
8.
CANOSSA
DSM
9.
ST. JOSEPH ITERAMBOGO SEM.
ZIWA MAGHARIBI
10.
CARMEL
MASHARIKI
4.2              Shule zilizoshika nafasi kumi za Mwisho
4.2.1         Shule za Serikali
NA
SHULE
KANDA
1.
MIHAMBWE 
KUSINI
2.
DINDUMA 
KUSINI
3.
KIROMBA 
KUSINI
4.
MARAMBO 
KUSINI
5.
MBEMBALEO 
KUSINI
6.
KINJUMBI 
KUSINI
7.
LITIPU 
KUSINI
8.
LUAGALA 
KUSINI
9.
MIGURUWE  
KUSINI
10.
NAPACHO 
KUSINI
4.2.2        Shule Zisizo za Serikali
NA.
SHULE
KANDA
1.
MFURU
MASHARIKI
2.
PWANI
MASHARIKI
3.
DORETA
KATI
4.
KIGURUNYEMBE
MASHARIKI
5.
RURUMA
KATI
6.
AT-TAAUN
MASHARIKI
7.
JABAL  HIRA SEM
MASHARIKI
8.
MKONO WA MARA
MASHARIKI
9.
KILEPILE
NYANDA KUSINI
10.
KIUMA
NYANDA KUSINI
5.0              UFAULU WA WANAFUNZI
Wanafunzi Walioshika Nafasi Kumi za Mwanzo
Na
JINA
JINSI
SHULE
1.
MAGRETH KAKOKO
KE
ST FRANCIS
2.
QUEEN MASIKO
KE
ST FRANCIS
3.
LUKUNDO MANASE
ME
KAIZIREGE
4.
FRANK J NYANTARILA
ME
KAIZIREGE
5.
GRACE MSOVELLA
KE
ST FRANCIS
6.
HARIETH MAKIRIYE
KE
ST FRANCIS
7.
ROBINNANCY MTITU
KE
ST FRANCIS
8.
HUMRATH LUSHEKE
KE
ST FRANCIS
9.
MUKHSIN HAMZA
ME
KAIZIREGE
10.
ANASTAZIA KABELINDE
KE
KAIZIREGE
6.0              HITIMISHO
Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Elimu ya Sekondari Kidato cha Pili mwaka 2012, yanaonesha kuwa kiwango cha ufaulu kimepanda kutoka asilimia 45.40 mwaka 2011 hadi kufikia asilimia 64.55 mwaka 2012. Aidha, watahiniwa 249,325 wataendelea na masomo ya kidato cha tatu mwaka 2013. Napenda kuwapongeza wanafunzi wote waliofaulu kuendelea na masomo na kuwataka kuendelea na bidii katika kujifunza.
Kwa upande mwingine, watahiniwa 136,946 ambao wameshindwa kupata wastani wa ufaulu wa alama 30 na wale waliofutiwa matokeo yao kutokana na udanganyifu watalazimika kukariri kidato cha pili mwaka 2013. Ni vema ikaeleweka kuwa kukariri kidato si adhabu bali ni kutoa fursa nyingine kwa mwanafunzi kuweza kupata maarifa, stadi na ujuzi wa elimu ya sekondari kidato cha kwanza na cha pili kwa kiwango kizuri. Hivyo ni matumaini yangu kuwa wanafunzi hawa watafanya bidii katika kujifunza na kuzingatia masomo ili waweze kufaulu, pia walimu kuwasaidia Wanafunzi hao waweze kufanya vizuri.
Serikali kwa upande wake itaimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi ya shule na kuziwezesha shule kukabiliana na changamoto mbalimbali kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji ikiwa ni pamoja na walimu kubadili mikakati ya ufundishaji na ujifunzaji na wazazi kufuatilia maendeleo ya wanafunzi.
Vilevile, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) itaendelea na jitihada zake za kuimarisha na kuboresha mazingira ya utoaji elimu bora kwa kujenga  maabara za sayansi, kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu, kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia na kuimarisha usimamizi wa shule. Aidha, wizara itaendelea kutoa walimu kwa awamu kila mwaka ili kukabiliana na upungufu uliopo.
Mhe. Philipo Mulugo (Mb)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
11/01/2013

10 comments:

Anonymous said...

matokeo yapo wapi?

Anonymous said...

mnatoa half details, hakuna matokeo hapo

Anonymous said...

Tallo

Anonymous said...

Maleba masuka

Anonymous said...

Mmatokeo yote ya jumla tunayaomba

Anonymous said...

Tunaomba matokeo ya shule zote ya mwaka 2012

Anonymous said...

tunaomba yote kwa ujumla

Anonymous said...

Naweza kupata matokeo ya kidato cha pili 2012

Anonymous said...

tumepata analysis lakn atujaona majina ya wanafunzi na shule zao

Anonymous said...

Matokeo mbona siyaoni yako wapi