Friday, January 11, 2013

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU TANO MKOANI RUVUMA

 Naibu waziri wa maji mhandisi Dkt Bilinith Mahenge akipanda kukagua tanki la maji safi na salama katika kijiji cha Ng'ombo wilayani Nyasa Ruvuma juzi lilijengwa kwa msaada wa fedha kutoka UNDB na halmashauri ya wilaya ya mbinga kwa zaidi ya shilingi 298 milioni
 Mbunge wa viti maalum mkoani Ruvuma mhandisi Stella Manyanya kushoto akimsisitia jambo Naibu Waziri wa maji mhandisi Bilinith Mahenge kulia wakati waziri huyo alipokuwa katika ziara yake wilayani Nyasa.
 Mhandisi wa maji wilaya ya Mbinga Evaristo Ngole kushoto akimfafanulia jambo Naibu waziri wa maji Mhandisi Dkt Bilinith Mahenge namna kukamilika kwa   ujenzi wa tangi la maji na huduma ya   maji katika kijiji cha Ng'ombo wilayani Nyasa ulivyokamilika ambapo utasaidia kupunguza tatizo kubwa la maji katika kijiji hicho.
Wakimsikiliza Naibu Waziri wa maji Mhandisi Bilinith Mahenge wakati akitoa maagizo kwake ya ufuatiliaji wa miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa katika wilaya hiyo.
 Naibu Waziri wa maji mhandisi Bilinith Mahenge kushoto akizungumza na wartumishi wa mamlaka ya maji safi nataka ya mji wa mbinga jana.
 Naibu  Waziri wa maji akielekeza jambo kwa viongozi wa wilaya ya Namtumbo mara baada ya kutembelea chanzo kimojawapo cha maji mjini Namtumbo hivi karibuni.
 Mkuu wa wilaya ya Namtumbo Abdul Lutavi akitoa maelezo kwa  Naibu Waziri wa maji mhandisi Bilinith Mahenge katikati kuzungumza na viongozi wa wilaya hiyo kulia ni mkurugenzi wa wilaya hiyo Mohamed Maje.
 Naibu Waziri wa maji akizungumza mara baada ya kuona mradi wa maji katika kijiji cha Peramiho A Wilayani Songea.
Naibu Waziri akiangalia mashine za kusukumia maji katika kijiji cha Peramiho.
 Naibu Waziri akitoa maagizo
 Naibu Waziri wa maji mhandisi Dkt  Bilinith Mahenge akiongea na wakazi wa kijiji cha Mkongotema songea vijijini mwishoni mwa ziara yake ya siku tano mjkoani Ruvuma kuangalia upatikana wa maji na kukagua miradi ya maji inayoendelea kujengwa mkoani humo.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu kushoto akizungumza na Naibu Waziri wa maji mhandisi Dkt Bilinith Mahenge kulia ofisini kwake jana wakati akiagana na Naibu waziri huyo
 Naibu Waziri akisalimina na akina mama wa kijiji cha mkongotema wilayani Songea ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji.
Naibu Waziri akizungumza wakati wa majumuisho ya ziara yake mkoani Ruvuma mjini Songea  na kuwataka viongozi wa mkoa huo kuwa makini hasa katika usimamizi wa miradi ya maji ambayo ndiyo inayochukua sehemu kubwa katika  maisha ya  kila siku ya binadamu kushoto mkuu wa wilaya ya Songea Josepph Mkirikiti na kulia mwenyekiti wa halmashauri wa wilaya ya songea vijijini.
Picha zote na Muhidin Amri wa Globu ya Jamii, Ruvuma

No comments: