Monday, December 24, 2012

JK ATOA MILIONI 30 KWA MRADI WA KULEA NA KUHIFADHI MBWA MWITU HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI MKOANI MARA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wasimamizi na wafadhili wa mradi huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na wawakilishi wa Kampuni  ya simu za mkononi ya Vodacom ambayo imechangia  dola za Marekani 450,000 kwa kipindi cha miaka mitatu ili kufanikisha mradi huo, ambao ulizinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka 2011. kushoto ni meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  akikata utepe katika boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu  kuashiria rasmi kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012 wakiwa nje ya  boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu akishuhudia kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.
 Mbwa mwitu wakirejea mbugani baada ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Bw. Joseph Kaboya, mhifadhi wa  boma maalumu la mradi huo  katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara, kwa kufanikisha zoezi hilo kwa mara ya pili. Kushoto ni meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga wa Taasisi ya Utafiti wa wanyama pori (TAWIRI).

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Mkurugenzi Mkuu wa Tawiri, Dkt. Simon Mduma (kushoto kwake) na meneja wa mradi huo Bw. Emmanuel Masenga baada ya sherehe hizo eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wa TANAPA Jumapili Desemba 22, 2012  wakielekea kwenye sehemu ya boma maalumu la kulea na kuhifadhi mbwa mwitu muda mfupi kabla ya kuachiwa huru kundi la pili la wanyama hao  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara. 

Wahifadhi wakifungua wigo wa senyenge  ili kuachia huru kundi la pili la mbwa mwitu  15 waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma hilo maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.

Mbwa mwitu hao 15 wakitoka katika hifadhin waliokuwa wamehifadhiwa kwa miezi kadhaa kwenye boma hilo maalumu la mradi huo,  lililojengwa katika eneo la Nyamuma, Magharibi mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mkoani Mara.PICHA NA IKULU.

No comments: