Sunday, December 16, 2012

AHADI ZA KUWASAIDIA WANAWAKE DHIDI YA UKATILI ZITEKELEZWE-TANZANIA


Na Mwandishi Maalum

Tanzania imeshauri na kupendekeza kwamba, mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Wanawake, (CSW57) pamoja na mambo mengine ujielekeze zaidi katika kuhakikisha kwamba ahadi ambazo zimekwisha kutolewa zinazolenga kumkomboa mwanamke dhidi ya ukatili vit zinatekelezwa.

Ushauri huo umetolewa na Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi, wakati wa mkutano wa siku mbili wa maandalizi ya Mkutano wa 57 wa CSW utakaofanyika kuanzia tarehe 4 hadi 15 Marchi mwaka 2013.

Ahadi ambazo Tanzania inataka zitekelezwe ni pamoja ile ya kuwapatia fursa ya elimu wanawake na watoto wa kike. Kwa kile ambacho, Mwakilishi huyo wa Tanzania amesema ni moja ya nyezo muhimu za kuliwezesha kundi hilo la jamii kukabiliana na kuepukana na aina zote za ukatili dhidi yao.

Balozi Manongi amesema katika mkutano huo wa siku mbili uliofayika mwishoni mwa wiki hapa Makao Makuu ya UM,kwamba Tanzania imekuwa ikiamini kwamba pamoja na mikakati mingine lakini fursa ya elimu wa wanawake na watoto kike ni nyezo muhimu zana.

Washiriki wa mkutano huo uliokuwa umeandaliwa na Tasisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya wanawake maarufu kama UN-WOMEN. Walikuwa ni wa kada mbalimbali wakiwamo Mawaziri, Mabalozi, wanazuoni, wanaharakati, na asasi zisizo za kiserikali. Kwamba Tanzania inaamini pamoja na mambo mengine fursa ya elimu kwa wanawake na watoto wa kike.

Wadau wa mkutano huo walipata fursa ya kuchangia mawazo yao na mapendekezo yao ili yaweze kusaidia katika maadalizi ya mkutano huo ambao huwashirikisha mawaziri wanaohusika na masuala ya jinsia, wanaharakati watafiti na vyama vya kiraia. Ni kati ya mkutano ambao huvutia wajumbe wengi hususani wanawake ukiacha mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

“ Tujiwekee malengo basi katika mkutano ujao kwamba, tunaweka mikakati itakayohakikisha ahadi zilizokwisha kutolewa huko nyumba zinatekelezwa. Kwetu sisi, Tanzania uzoefu umetuonyesha kwamba fursa ya elimu kwa wanawake na watoto wa kike inawawezesha kujipambanua, kujitambua lakini pia kuzijua na kuzitafuta haki zao pamoja na fursa za kujiinua kiuchumi” akasisitiza Balozi Manongi.

Wito huo wa kutilia mkazo wa utekelezaji wa ahadi na husususani elimu, uliungwa mkono na wajumbe wengi akiwamo katibu Mkuu Msaidizi na Mkurugenzi Mtendaji wa UN-WOMEN Bi Michelle Bachelet.

Bi. Bachelet alisema hapana shaka kwamba wajumbe wengi wanakubaliana kuwa elimu ni moja ya nyezo muhimu katika kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake na watoto wakike na kwamba elimu pia inatakiwa kutolewa kwa wanaume na wadau wengine ili nao wawe sehemu ya mapambano hayo.

Mkutano huo utafanyika ikiwa na mwaka mmoja baada ya wajumbe wa mkutano wa 56 uliofanyika mwezi Marchi mwaka huu , hapa kushindwa kutoka na Tamko la mwisho, baada ya wajumbe wa nchi zinazoendelea na wale wan chi zilizoendelea kushindwa kukubaliana na kufikia muafaka kuhusu kuingozwa kwenye Tamko hilo suala ya kutambua ndoa za jinsia moja.

Kutopatikana kwa Tamko hilo kwa namna moja ama nyingine kuliadhiri hata mambo mengine ya msingi na muhimu yaliyokuwa yanalenga kumsaidia mwanamke likiwamo suala la kilimo.

Ili kujaribu kuepusha kile kilichotekea katika mkutano wa 56 ndiyo maana kumekuwapoa na maandalizi ya awali kama mkutano huu wa wadau uliofanyika mwishoni mwa wiki.

No comments: