Muonekano wa gamba la nje wa kitabu kilichoandikwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Balozi Juma Mwapachu na kuzinduliwa ndani ya hotel ya New Africa mwishoni mwa wiki.
Pichani kulia ni Mgeni rasmi wa hafla fupi ya uzinduzi wa kitabu,Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa nchi za Afrika,Dkt Salim Ahmed Salim akikata utepe kuashira uzinduzi wa kitabu kilichoandikwa na Balozi Juma Mwapachu kama kionekanavyo juu pichani,chenye ya kurasa 414.
Baada uzinduzi kufanyika walipeana mikono ya pongezi kwa kazi nzuri iliyofanyika
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa nchi za Afrika,Dkt Salim Ahmed Salim,akizunguma mbele ya baadhi ya wageni waalikwa (hawapo pichani) waliofika kushuhudia uzinduzi wa kitabu hicho,aidha katika uzinduzi huo Dkt Salim Ahmed Salim alieleza kwa kuwataka Wana Afrika Mashariki kuandika vitabu ili historia ya Afrika iandikwe na Waafrika wenyewe katika muktadha halisi.
Mwandishi wa kitabu hicho,aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Balozi Juma Mwapachu akizungumza mbele ya wageni waalikwa wakiwemo na baadhi ya Wanahabari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa kitabu chake kilichozungumzia Uwekezaji,soko la pamoja,taasisi za wanachama wapya-Rwanda na Burundi,ambacho pia kimeweka wazi changamoto kama bajeti tegemezi,kushindwa kuleta maingiliano ya wananchi na kuwapo na hofu ya mtangamano kwa baadhi ya wanachama,Balozi Mwapachu alisema kuwa mnunuzi Mkuu Serikali imeacha kununua vitabu na kusababisha waandishi kukosa motisha ya kuandika,aliongeza kuwa Serikali haitumii rasilimali za kutosha kununua vitabu,hata wale wanaotaka kuandika hawaandiki tena kwani hakuna soko,Aidha pia aliishauri sekta binafsi kutoa motisha kwa waandishi wa vitabu,kwamba wanapotoa mchango wa maendeleo ya jamii kwenye elimu watenge kwa ajili ya waandishi wa vitabu ili kuamsha ari ya uandishi.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa nchi za Afrika,Dkt Salim Ahmed Salim,akizungumza jambo na Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini (CHADEMA),Mh.Zitto Kabwe mara baada ya uzinduzi kufanyika.
Kutoka kulia ni ,aliyekuwa Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),Balozi Juma Mwapachu,Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman pamoja na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa nchi za Afrika,Dkt Salim Ahmed Salim wakiwa wameketi wakisubiri hafla ya uzinduzi wa kitabu.
Pichani shoto ni Mh.Sir George Kahama,Profesa Mkandala,Dkt Salim Ahmed Salim pamoja na Balozi Juma Mwapacha wakijadiliana jambo kabla ya uzinduzi kufanyika.
Pichani juu na chini ni Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo ya uzindui.
Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa nchi za Afrika,Dkt Salim Ahmed Salim akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa,
Baadhi ya wadau mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi huo
No comments:
Post a Comment