Amana Bank
inajivunia kuwa benki ya kwanza kabisa ya Kiislam nchini Tanzania ikiwa na
malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee ambazo zinafuata
Sharia kikamilifu kwa kuzingatia maadili na kwa njia iliyowazi na kwa kutumia
teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja wetu wote.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Amana Bank,
Bw. Haroon Pirmohamed akitoa historia
fupi ya benki alisema, “Historia ya kuanzishwa kwa Amana Bank, inaanzia mwezi
October mwaka 2009 ambapo baadhi ya wafanyabiashara walikutana na kupanga
mikakati ya kuanzisha benki ya kiislam nchini Tanzania isiyofuata misingi ya
riba. Benki ilipata leseni ya muda kutoka Benki Kuu ya Tanzania tarehe 4
Februari 2011 na kusajiliwa rasmi tarehe 25 Februari 2011 ikiwa na mtaji
ulioidhinishwa wa Shilingi za Kitanzania Billioni 100 na uliolipiwa kiasi cha
shilingi za kitanzania Billioni 21.5”.
Aliendelea
kusema kuwa, “katika mwaka mmoja Amana Bank imeweza kufungua matawi matatu jijini
Dar es Salaam. Matawi hayo ni
Tandamti lililoko eneo la Kariakoo, Nyerere Road Branch, lililopo barabara ya Nyerere
na Main Branch lililopo katikati ya jiji katika jengo la Golden Jubilee Tower”.
Benki
inatoa huduma na bidhaa ambazo zinafuata misingi ya Sharia za kiislam na ambazo
zimepitishwa na Bodi ya Sharia. Bidhaa na huduma zinazotolewa na benki si kwa
ajili ya jamii ya kiislam pekee bali kwa watu wote ambao wanaamini katika mfumo
wa kibenki usiofuata misingi ya riba. Huduma za Amana zinatolewa kwa makampuni
na watu binafsi. Huduma zinazotolewa ni pamoja na:-
Akaunti
za Akiba ambazo zinajumuisha Akaunti ya watoto (Nuru Akaunti), Akaunti ya
wanawake (Annisa Akaunti), Akaunti ya akiba kwa ajili ya nyumba za ibada
zilizosajiliwa (Ihsan Account) pamoja na Akaunti ya Hijja (Hajj Account). Pia
benki ina Akaunti za hundi na Akaunti za biashara. Vilevile benki ina akaunti
ambazo ni maalum kwa ajili ya makampuni mbalimbali. Benki pia ilianzisha huduma
ya ulipaji wa kodi za mapato na ushuru wa fordha kupitia matawi yake. Wateja na
wasio wateja sasa wanaweza kulipa kodi hizi katika matawi ya Amana Bank. Pia
benki ilianzisha huduma ya kutuma fedha popote duniani kupitia huduma ya
Western Union. Benki ina lengo la kumfanya mteja anapoingia katika matawi yetu apate huduma
zote mahali pamoja (one-stop shop).
“Mpaka
tarehe 25 Novemba mwaka huu, Amana imefanikiwa kuwa na jumla ya akaunti 4093 na akiba zaidi ya Shilingi Bilioni
35”, alisema Mwenyekiti Bw. Haroon Pirmohamed.
Ni
kwa kutumia teknolojia hii ya kisasa Amana Bank ilizindua huduma ya Amana
Mobile ambayo inaenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia duniani. Amana
Mobile ni huduma za kibenki kwa kutumia mtandao wa internet na simu za
mkononi.” “Huduma hii inalenga
kuwarahisishia wateja wetu kufanya miamala na kupata huduma mbalimbali ambazo
zinatolewa na benki yetu kwa njia ya mtandao. Lengo la kuanzisha huduma hii ni kurahisisha
usimamizi wa akaunti za wateja wakati wowote, popote walipo siku saba za wiki”
alisema mwenyekiti.
Kwenda
mbele, uongozi wa benki unafanya jitihada kubwa kuboresha nafasi ya benki
katika soko na pia kusambaa sehemu nyingine nchini. Benki inatarajia kufungua
matawi matatu mwanzoni mwa mwaka 2013 katika mikoa ya Arusha na Mwanza na tawi
la pili katika eneo la Kariakoo mtaa wa Lumumba. Pamoja na ufunguzi wa matawi, Amana
Bank pia inajipanga kuboresha huduma zake na pia kuongeza huduma zingine.
Tunawakaribisha
wote kufungua akaunti Amana Bank. Karibuni katika ulimwengu mpya kabisa wa
kibenki, unaofuata Sharia kikamilifu.
Kwa
maelezo na taarifa zaidi unaweza kupata kupitia tovuti yetu ya www.amanabank.co.tz
No comments:
Post a Comment