Serena Hotel - Dar es salaam,
Tarehe :
18 / Oktoba / 2012
Amana Bank,
Benki ya kwanza Tanzania inayofuata Sharia kikamilifu, leo tunazindua huduma ya
“Amana Mobile”.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Biashara (Amana Bank)
Bw. Sudi Marungu alisema Dar es salaam
kuwa “ Amana Mobile ni huduma za kibenki kwa kutumia mtandao wa internet na simu
zamkononi.” “Huduma hii inalenga kuwa rahisishia wateja wetu kufanya
miamala nakupata huduma mbalimbali ambazo zinatolewa na benki yetu kwa njia ya mtandao. Lengo la kuanzisha huduma hii nikurahisisha usimamizi
wa akaunti zawateja wakati wowote, popote walipo siku saba za wiki.”
Akizungumzia
kwa ufupi juu ya huduma hii Bw. Sudi Marungu alisema,
“ Amana Bank inajivunia kuwa benki ya kwanza
kabisa ya Kiislam nchini Tanzania ikiwa na malengo ya kutoa huduma za kibenki za
kisasa na za kipekee ambazo zinafuata Sharia kikamilifu kwakuzingatia maadili na
kwa njia iliyowazi na kwakutumia teknolojia ya kisasa kwamanufaa ya wateja wetu
wote.”
Hata
hivyo, alisema ni kwa kutumia teknolojia
hii ya kisasa Amana Bank leo hii inazindua huduma ambayo inaenda sambamba na maendeleo
yakiteknolojia duniani. Mteja wa sasa anahitaji kufikiwa na huduma za ki benki popote
pale alipo wakati wowote.
Amana Mobile
itapatikana kupitia simu za mkononi na wateja ambao wameunganishwa na mitandao yote
ya simu wanaweza kutumia huduma hii.
Wakati huduma
za kibenki kupitia mtandao yaani “Internet
Banking” zinaweza kufanyika kupitia kompyuta
ambazo zimeunganishwa namtandao wa internet. Huduma hizi ni zaharaka na rahisi hivyo
humuwezesha mteja kufanya miamala ya kibenki popote alipo kwa wakati anaotaka. Amana
Mobile inalenga kutoa huduma mbalimbali za kibenki kupitia simu za mkononi.
Kupitia
Amana Mobile wateja wetu wataweza kuuliza salio la akaunti zao, kupata taarifa fupi
na taarifa kamili za akaunti zao, Kununua muda wa maongezi kwa mitandao yote ya
simu zamkononi, Kufanya malipo ya awali na Ankara kama vile kununua LUKU, kulipa bili za DAWASCO, Star Times, TTCL Broadband,
Uhuru one, DSTV nakadhalika. Pia Amana Mobile inamuwezesha mteja
kuomba kitabu cha hundi, kuhamisha fedha kutoka akaunti moja kwenda nyingine ndani
ya benki au kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti yake kwenda kwenye akaunti yake
ya simu ya mkononi kama vile M-pesa,
TigoPesa na Airtel Money.
Kwa upande
mwingine Amana Internet Banking inarahisisha usimamizi wa akaunti za wateja wetu
kwani wanaweza kufanya miamala yakibenki popote pale walipo duniani..
Moja ya faida
kubwa ya huduma hii nikwamba inatoa urahisi wakufanya miamala ya kibenki kwa muda
ambao mteja anahitaji huduma hiyo iwe ofisini, nyumbani, safarini au hata akiwa
nje ya nchi. Huduma hii imerahisisha miamala midogo midogo ambayo hapo awali iliwalazimu
wateja wetu kufika katika matawi yetu kupata huduma sasa kupata huduma popote walipo,
kwa urahisi na haraka.
Hii ni hatua
kubwa kwa Amana Bank hasa ikizingatiwa kuwa benki ina miezi kumi tu tangu ilipoanza
kutoa huduma kwa wateja. Tunawakaribisha wote kufungua akaunti Amana Bank.
Kwa maelezo na taarifa
zaidi unaweza kupata kupitia tovuti yetu
ya www.amanabank.co.tz.
Asanteni
No comments:
Post a Comment