Kamishna
kutoka Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw.
Christopher Shekiondo akizindua rasmi maonyesho ya sanaa ya Sober House
jijini Dar amesema kwa niaba ya tume ya kudhibiti dawa hizo Zanzibar na
kwa Serikali kwa ujumla wanatambua mchango wa wadau mbalimbali
uliosaidia vijana kuachana na tabia hiyo na kuahidi kushirikiana nao
katika kuhakukikisha asilimia kubwa ya vijana wanabadilika kwa kutumia
njia mbalimbali ikiwemo sera madhubuti za Serikali na mipango mikakati
ikiwemo utekelezaji wa Kampeni za ufahamu wa madhara ya madawa hayo.
Ameongeza
kusema kuwa mikakati ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya
inakabiliana na changamoto nyingi kutokana na uhaba wa vituo na
wataalamu lakini Serikali haijakata tamaa na inaahidi kutimiza lengo
hilo katika muda muafaka ikishirikiana na wadau mbalimbali na kuomba
wadau wengine wajitokeze.
Mkurugenzi
wa Alliance Francaise Tanzania Bw. Sullivan Benetier akitoa hotuba ya
kumkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya sanaa ya Sober
House Zanzibar ambapo amesema wao wamekuwa wadau wakubwa wa kusaidia
mpango wa kuwawezesha vijana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na
kujirudi na kutumia vipaji walivyonavyo kufanikisha maisha yao na
kujipatia kipato.
Baada
ya kufanikiwa kwa mpango wa kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi
sasa wamejikita katika kuhakikisha vijana Tanzania wanaachana kabisa na
wimbi la matumizi ya dawa za kulevya kwa kuunga mkono shughuli hii
ambapo vijana walioonyesha mfano kwa kubadili tabia wanapata fursa ya
kuonyesha sanaa zao za kuchora na kuchonga na pia kutokuwa na vipindi
vingine vya kutoa ushauri nasaha wa kiakili utakowasaidia kujitambua na
kuwafanya kuwa mabalozi watakaoelimusha vijana wenzao kuachana na tabia
za matumzi ya dawa hizo.
Mgeni
rasmi katika maonyesho ya Sanaa ya 'Sober House' yaliyozinduliwa jijini
Dar es Salaam Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya visiwani
Zanzibar Dkt. Shekiondo (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na
wadau wanaondesha mkakati wa kuwasaidia vijana kubadili tabia na
kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na badala yale kuonyesha vipaji
walivyo navyo katika sanaa.
Muasisi
wa Sober House Visiwani Zanzibar Bw. Suleiman Maulid akitoa shukrani kwa
niaba ya wenzake ambapo ametoa wito kwa vijana wote Tanzania
wanaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya kuachana na tabia hiyo na
kisha kujiunga na Sober House kwa msaada zaidi wa kimawazo, kifikra na
kielimu. Pia ameitaka Serikali kuongeza nguvu zaidi kwa taasisi
zinazopambana na dawa za kulevya nchini katika kuwawezesha kufanikisha
mipango ya kuwawezesha vijana kujirudi.
Mkurugenzi
wa Chama cha maafisa Ustawi wa Jamii Bi. Anna Swai akionyesha Sanamu
ya Msanii Mkongwe nchini Bi. Kidude iliyotengenezwa na mmoja wa vijana
waliobadili muelekeo na kuamua kuachana na dawa za kulevya Zakaria Mwiru
(kushoto) wakati wa ufunguzi wa kazi za sanaa
Baadhi
ya Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa Maonyesho ya Sanaa ya Sober
House Recovery yanayoendelea katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini
Dar na kiingilio ni Bure kwa wote.
Raia
wa kigeni akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na vijana
waliobadilika na kuamua kuacha tabia za utumiaji wa madawa ya Kulevya na
kujishughulisha na sanaa.
Mbunifu
wa Mavazi nchini na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija
Mwanamboka a.k.a Kubwa la Maadui alikuwa ni miongoni mwa wageni
waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.Pichani akipozi na moja ya
mkoba uliosukwa na mkeka ikiwa ni kazi za vijana waliokuwa wakitumia
madawa ya kulevya na kujifunza fani mbalimbali na mwishowe kuvionyesha
kwa jamii.
Khadija
Mwanamboka akichukua taswira katika moja ya picha zilizoonekana
kumvutia wakati wa maonyesho ya Sober House Art Exhibition yanayoendelea
katika Ukumbi wa Utamaduni wa Ufaransa Alliance Francaise wa jijini
Dar.
Maonyesho
haya ni bure, Tujitokeze kuwaunga vijana wetu walioamua kubadili tabia
na tujifunze kutoka kwao. "Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana".
Kijana
Zakaria Mwiru akionyesha ubunifu wake wa kinyago chenye taswira ya
Msanii maarufu wa muziki wa taarab hapa nchini Bikidude ambayo
ilimchukua muda wa wiki moja kutengeneza na alifanya hivyo kutokana na
kuvutiwa na kazi za muziki za msanii huyo zilizoenea kote visiwani
Zanzibar na kuamua kuchonga kinyago hicho. Kinyago hichi kilianza
kupigwa mnada kwa Dola 550 mwenye kuvutiwa nacho ajitokeze.
Kazi ya mikono ya Zakaria Mwiru. Pichani ni Sanamu ya Bi.Kidude.
Pichani
Juu na Chini ni kazi za Ubunifu zilizofanywa na Vijana waliobadili
mwelekeo wa maisha waliopo katika taasisi ya Sober House ya visiwani
Zanzibar.
Kamishna kutoka Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw.
Christopher Shekiondo (kushoto) akionekana kuvutiwa na moja ya sanamu
ilyotengenezwa na vijana waliobadili mwelekeo na kuamua kuachana na dawa
za kulevya na kuendeleza vipaji vyao ikiwemo sanaa ya uchongaji. Ahmed
Awadhi
Mkurugenzi
wa Alliance Francaise Tanzania Bw. Sullivan Benetier (kulia)
akibadilishana mawazo na Mbunifu wa Mavazi nchini ambaye pia Balozi wa
Sober House visiwani Zanzibar Ally Rehmtullah (katikati) pamoja na
Mwasisi na CEO wa Missie Popular Blog Mariam Ndabagenga.
Wadau
waliohudhuria Uzinduzi wa Maonyesho ya Sanaa yaliyoandaliwa na Sober
House Zanzibar yanayoendelea katika Ukumbi wa Alliance Francaise wa
jijini Dar es Salaam na kiingilio ni bure.
No comments:
Post a Comment