TUACHE MALUMBANO
TUJADILI HALI HALISI- MANONGI
Na Mwandishi
Maalum
Wakati Baraza
la Uchumi na Fedha ( ECOSOC) la
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, likizindua Tathmini ya Miaka Minne
ya Shughuli za Maendeleo ya Umoja wa Mataifa ( QCPR). Tanzania imetaka majadiliano ya tathimini hiyo yalenge zaidi
katika kujadili hali halisi ya mambo badala ya nchi kujitafutia umaarufu.
Akichangia majadiliano hayo Mwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi amesema, tathimini hiyo
inafanyika katika kipindi ambacho mdororo wa uchumi ukiendelea kuitikisa dunia
na kiwango cha umaskini kikiongezeka.
“ Mengi
yamekwisha kuzungumzwa na wasemaji walionitangulia kuhusu tathmini hii. QCPR
inajadiliwa wakati mtikisiko wa uchumi
ukiendelea duniani na umaskini ukiongezeka. Na pia tunashuhudia
kushuka kwa kiwango cha misaada ya maendeleo inayotolewa kwa nchi zinazoendelea. Hebu basi na tutumie
majadiliano haya kujadili ukweli halisi
wa mambo yalivyo badala ya kujadiliana
nafasi ya nchi au umaarufu wa nchi”.Akasisitiza Balozi Manongi.
Tathimini
hiyo ya miaka minne ambayo inalenga katika kupitia utekelezaji wa mipango ya
maendeleo zikiwamo será mbalimbali
itahusisha Mashirika, Taasisi na
Mifuko iliyochini ya Umoja wa Mataifa na
ambayo kwayo imekuwa ikitumika kufadhili miradi na programu mbalimbali za
Maendeleo.
Mashirika na Taaisisi hizo 11
ikiwamo miradi ya utafiti na mafunzo
ni pamoja UNDP, UNICEF, WFP. UNHCR. UNCTAD na UNEP.
Balozi Manongi amesema Tanzania inapenda kusisitiza umuhimu wa mipango
ya Umoja wa Mataifa katika ngazi
ya nchi, mipango ambayo hususani ile ambayo imeainishwa na nchi zenyewe.
“ Mipango hii yote inalenga katika kutusaidia sisi
katika kukabiliana na changamotoz zetu.
Mwezi June mwaka jana, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana
na Umoja wa Mataifa ilizindua Mpango wa
Misaada ya Maendeleo ( UNDAP). Mpango
huu unaelezea ushirikiano wetu na Mashirika 20 ya UM ikiwamo Mifuko na Programu katika maeneo ya ukuaji wa uchumi
na upunguzaji wa umaskini, uboreshaji wa maisha, ustawi wa jamii,
utawala bora, masuala ya dharua na udhibiti wa maafa na uhifadhi wa wakimbizi”
akabainisha
Na kuongeza kwamba Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo umefarijika sana kwamba QCPR inafanyika sanjari na kilele cha mpango
wa majaribio wa Ufanyaji kazi wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa (
Delivering
as One).
“ Ni matumaini yetu kwamba matokeo ya utafiti wa tathmini huru ya
DaO itaendelea kutujulisha kuhusu mchakato wa mapitio. Jambo moja ni
wazi kwamba nchi ambazo zimejitolea kutekeleza mpango huu zingependa kuudumisha
na kuendelea nao”. Akasisitiza Balozi
Na kuongeza kwamba tangu kuanza kwa majaribio mwaka 2007 nchi nyingi zimeukubali na
litakuwa jambo la kusikitisha kama QCPR haitautilia maanani.
Aidha kama ilivyokuwa kwa wasemaji wengine, Tanzania
pia ilirejea wito wake wa kutaka kuimarishwa kwa Ofisi ya Mratibu Mkazi ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa
ukamilifu. Huku ikisisitiza kwamba mafanikio ya utekelezaji wa DaO ishuke hadi
katika ndani ya Umoja wa Mataifa.
Aidha Tanzania
pamoja na mambo mengine imesisitiza haja na umuhimu wa uboreshaji wa njia za
utekelezaji wa DaO. Na kwamba anatoa wito wa Bodi zote zinazosimamia Mashirika,
Mfuko na Programu kupitia mifumo yao ya utendaji kwa lengo la kuimarisha uratibu na
ushirikiano ili kupunguza gharama.
Awali akizindua Tathimini hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa UM,Bw. Jan
Eliason alitoa changamoto kwa Umoja huo
kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia hali halisi ilivyo hivi sasa.
Akasema
“ mazingira ya changamoto za maendeleo yamebadilika, mataifa mengi yanazidi kutambua kuwa chombo hiki kinahitaji kutekeleza wajibu wake vizuri zaidi
kwa kushughulikia matatizo mtambuka ya
kiuchumi, kijamii na kimazingira”
akasema na kuongeza “ ni miaka michache
tu iliyopita ambapo zaidi ya nusu ya
nchi ambazo hivi sasa zinatambuliwa kama nchi zenye uchumi wa kati, zilikuwa ni
nchi ambazo uchumi wake ulikuwa mdogo”.
Na kwa sababu hiyo anasema kwamba
wakati UM ukizindua tathimini hiyo ya maiaka minne ya shughuli zake za maendeleo,
lazima itambue kwammba maendeleo endelevu ndiyo nguzo na kiini katika kipindi
hiki ambacho idadi ya wadau wa
ushirikiano wa maendeleo wakiongezeka.
“
Hivi sasa ushirikiano wa kimaendeleo siyo tena uwanja unaohodhiwa na nchi Fulani au mashirika ya kimataifa”
akasema na kusisitiza “ hivi sasa
tunategemea zaidi michango ya sekta binafasi,
mifuko ya kijamii, wanazuoni
na vyama vya kijamii. Mfumo wa Umoja wa Mataifa
unatakiwa kuanza kubuni njjia mbadala na sahihi za kuunganisha nguvu za wadau
hawa wapya”.
No comments:
Post a Comment