Mgeni Rasmi katika Hafla ya Kuwakaribisha Warembo wanataoshiriki kinyang'anyiro cha kumsaka Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 katika Mji wa Monduli,Mama Regina Lowassa akiwaasa warembo hao juu ya wao kujiheshimu na kuliheshimu shindano hilo.
Mkurugenzi wa Rino Agency ambao ni waandaaji wa Mashindano ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya E'Manyata,Monduli.Kulia kwake ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo,Mama Regina Lowassa,Dada Mkubwa wa Mh. Lowassa Mama Kalaine Lowassa pamoja na Meya wa Monduli,Mh. Kadogoo.
Dada mkubwa wa Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa,Mama Kalaine Lowassa (kulia) pamoja na Mke wa Mh. Lowassa,Mama Regina Lowassa wakishirikiana kwa pamoja kuwavisha mavazi ya kimasai warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 waliotembelea Mji wa Monduli,jijini Arusha.
Muwezeshaji wa Ziara ya Miss Tanzania Wilayani Monduli,Robert "Bob" Lowassa akivishwa vazi la kimasai na Shangazi yake,Mama Kalaine Lowassa ikiwa ni pongezi kwake kwa kuwezesha Warembo hao kufika kwenye Mji huo.
Warembo wakiwa wamevalia Mavazi ya Kimasai.
Kina Mama wa Jamii ya Kimasai.
Viongozi wakuu wa Kamati ya Miss Tanzania,toka kushoto ni Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania,Albert Makoye,Afisa Habari wa Miss Tanzania,Ricco Hiden,Katibu Mkuu wa Miss Tanzania,Bosco Majaliwa pamoja na Miss Tanzania 2012,Salha Israel.
Miss Tanzania anaeshikilia taji hilo hivi sasa,Salha Israel akiwa pamoja na Washiriki wenzake wa Mwaka jana,Jennifer Kakolaki (kulia) na Irene Karugaba ambaye ndie Matron wa warembo hao kwa sasa.
Mgeni Rasmi,Mama Regina Lowassa akicheza Kwaito sambamba na Warembo wa Redd's Miss Tanzania.Mwenye Shati nyeupe ni Muwezeshaji wa Ziara ya Miss Tanzania Wilayani Monduni,Robert "Bob" Lowassa.
Mmoja wa Warembo wa Redd"s Miss Tanzania kutoka Kanda ya Ziwa,
Mgeni Rasmi,Mama Regina Lowassa akiwa na Uongozi wa Kamati ya Miss Tanzania na Viongozi wa Mji wa Monduli pamoja na Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012.
Baadhi ya Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012,wakishiriki kucheza Mchezo wa Mpira wa Wavu wakatika walipowatembelea watoto waishio kwenye Mazingira magumu waliokuwepo kwenye Shule ya Arusha jijini humo.
Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2012 wakishiriki kucheza mpira wa Miguu na Watoto Yatima kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Arusha.
kuvuta kamba.
Warembo wakishiriki kuosha magari ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha wakazi wa jiji la Arusha kuwachangia fedha kwa ajili ya mahitaji mbali mbali watoto yatima wa Jijini humo.
No comments:
Post a Comment