Monday, August 27, 2012

Taswira Mbalimbali Za Katibu Mkuu wa Chadema Dk Wilbrod Slaa Kwenye Mkutano wa Kuwashukuru Wananchi wa Jimbo la igunga Posted: 26 Aug 2012 12:38 PM PDT Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akisalimiana na aliyekuwa mgombea wa ubunge jimbo la Igunga katika uchaguzi mdogo mwaka jana, kupitia Chadema, Mwalimu Joseph Kashindye, walipokutana katika mkutano wa kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, ambayo Chadema kiliibuka mshindi, uliofanytika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa akikumbatinana na Mbunge wa Maswa Mashariki, Slyvester Kasulumbai, walipokutana katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi wa jimbo la Igunga kwa ushiriki wao katika kesi ya uchaguzi wa jimbo hilo, kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Igunga juzi. Kutokana na kilichoelezwa kuwekwa kwa lami chini yakiwango katika mlima Sekenke mkoani Singida, imeharibika vibaya kama inavyoonyesha pichani magari yakipita kwa shida baada ya lami hiyo kubomoka kwa kipindi kifupi tangu iwekwe, kama ilivyokutwa jana.Picha na Joseph Senga Rais Jakaya Kikwete pamoja na familia yake ameshiriki kikamilifu katika zoezi la kitaifa la sensa ya maendeleo ya watu na makazi{VIDEO} Posted: 26 Aug 2012 12:29 PM PDT MKUU WA WILAYA YA TANGA ATEMBELEA TIMU NZIMA YA SERENGETI FIESTA 2012 Posted: 26 Aug 2012 12:30 PM PDT Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (kushoto) akiongea machache mara baada ya kutembelea timu nzima ya Serengeti Fiesta 2012. Ambapo Mkuu huyo wa wilaya alisisitiza watu wajitokeze kwa wingi uwanja wa Mkwakwani kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012 huku akitoa msisitizo kwa wakazi wa Tanga kujitokeza katika zoezi la sensa. Tamasha la Serengeti Fiesta linatarajiwa kufanyika leo tarehe 26.8.2012 Baadhi ya wageni wakimsikiliza kwa makini mkuu huyo wa wilaya ya Tanga. Afisa Mausiano wa Clouds Media Group, Simon Simalenga akitoa msisitizo wa jambo mbele ya mkuu wa vipindi wa Clouds Fm Sebastian Maganga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego. Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego (katikati) akiwa katika picha na timu ya Serengeti Fiesta 2012 pamoja na wageni. Chadema Kimemtaka Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye Kukiomba Radhi Chama Hicho ndani ya Siku Saba na Kulipa Fidia ya Shilingi Bilioni Tatu {VIDEO} Posted: 26 Aug 2012 12:17 PM PDT John Mnyika:Chadema imeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kufuatia madai ya uzushi na uongo aliyoyatoa tarehe 12 Agosti 2012 Posted: 26 Aug 2012 12:15 PM PDT Mbunge wa Ubungo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi.Picha na Francis Dande --- Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kufuatia madai ya uzushi na uongo aliyoyatoa tarehe 12 Agosti 2012 kuwa anao ushahidi kwamba CHADEMA kimekuwa kikiwahadaa wananchi kwa kuwachangisha fedha huku kikipokea mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili kutoka nje. Izingatiwe kuwa matamshi yake yalitangazwa na vyombo vya habari vya kielekroniki ikiwemo vituo vya televisheni, radio na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii tarehe 12 Agosti 2012 na katika kurasa za mbele za magazeti mbalimbali tarehe 13 Agosti 2012. Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA iliagiza wanasheria wamwandikie barua ya kumtaka kukiomba radhi Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kutumia njia ile ile aliyotumia kufanya propaganda chafu za kuikashifu na kuifitisha CHADEMA kwa umma wa watanzania ikiwemo kuzusha kuwa upo uwezekano wa CHADEMA kupewa fedha hizo kwa mikataba yenye masharti ya kuiweka nchi rehani. Tayari ameshaandikiwa barua ya kisheria tarehe 24 Agosti 2012 ya kumtaka aombe radhi na kulipa fidia ya bilioni tatu kwa matamshi hayo ya uzushi na uongo yenye maana ya kuwapotosha waliyoyasikia na kuyasoma kuwa CHADEMA kinawalaghai wananchi, kina viongozi wasio waaminifu na kwamba kiko tayari kuuza nchi wa uroho wa madaraka. Kipaumbele cha CHADEMA katika suala hili ni kuombwa radhi hata hivyo kiwango cha fidia ya fedha kwa fedheha kilichotakiwa ni fundisho kuwa uzushi na uongo unagharimu. Ikumbukwe kwamba tarehe 12 Agosti 2012 nilitoa kauli ya awali baada ya mkutano Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine nilieleza kwamba tutatoa tamko la kueleza hatua za ziada baada ya kupata taarifa kamili aliyoitoa. Katika kauli hiyo nilitoa mwito kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kueleza watanzania iwapo propaganda hizo chafu zina baraka zake; hivyo ukimya wake mpaka sasa kuhusu matamshi hayo inakifanya CHADEMA kuwa na imani yenye shaka (benefit of doubt) kwamba Nape hakutumwa na chama chake kutoa matamshi aliyoyatoa. CHADEMA inachukua fursa hii kuutaarifu umma kwamba asipotekeleza matakwa hayo ndani ya siku saba kuanzia tarehe hiyo aliyopokea barua hatua nyingine ya kumfikisha mahakama kuu zitaanzishwa ili aweze kuchukuliwa hatua zaidi. Pamoja na kuchukua hatua za kisheria, CHADEMA kinaendelea kutimiza dhima yake ya kuleta uongozi bora, sera sahihi, mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya Tanzania kwa pamoja na mikakati mingine kutekeleza operesheni ya vuguvugu la mabadiliko nchini (M4C) na tunawashukuru wananchi kwa kuendelea kuunganisha nguvu ya umma kwa hali na mali katika maeneo mbalimbali nchini. Imetolewa tarehe 26 Agosti 2012 na: John Mnyika (Mb) Mkurugenzi wa Habari na Uenezi IKULU:Rais Jakaya Kikwete na Familia Yake Washiriki Zoezi la Sensa na Makaazi Posted: 26 Aug 2012 12:11 PM PDT Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mkewe Mama Salma Kikwete na familia yake akijibu maswali toka kwa karani wa sensa ya wazu na makazi Bw. Clement Ngalaba leo Agosti 26, 2012 wakati alipojiunga na mamilioni ya Watanzania katika zoezi hilo lililofanyika kwa mafanikio makubwa nchi nzima.Picha na IKULU Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein na Familia Yake Washiriki Zoezi la Sensa ya Watu na Makaazi Posted: 26 Aug 2012 12:08 PM PDT Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Moahmed Shein, akijiandikisha na familia yake kwa Karani Asia Hassan Mussa, (kushoto) katika zoezi la Sensa ya Watu na Makaazi, lililoanza leo nchini kote,Rais akiwa katika Shehia ya Migombani Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,(kulia ) Mke wa Rais Mama Mwanamwema Shein.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar Baadhi ya Taswira Za Mkutani wa Chadema Reading Nchini Uingereza Posted: 26 Aug 2012 12:05 PM PDT Dr Alex akiongea kwenye mkutano wa Chadema Reading Nchini Uingereza Leo Sehemu ya wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye mkutano wa CHADEMA Reading Nchini Uingereza Leo.Picha zaidi Baadae AUDITION YA 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' YAVUTA WASHIRIKI ZAIDI YA 100 JIJINI DAR


Ally Rehmtullah.
Casting Coordinator wa ALLY REHMTULLA'S COLLECTION 2012 Audition Martin Kadinda akitoa mwongozo wa zoezi hilo kwa Models walioshiriki.
Baadhi ya Models wa kiume waliojitokeza Serena Hotel wakisubiri usaili.
Pichani Juu na Chini ni Models wa kike na wa kiume wakipita mbele ya Majaji wakati wa usaili.
Meza kuu ya Majaji kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Alliance Auto Bw. Alfred Minja akiwakilisha CFAO Motors wauzaji wa Magari ya Mercedes Benz ambao ndio wadhamini wakuu wa 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013', Aysha Mbarak Meghji kutoka Ayman Garage-Convolution Ideas Ltd, Administrative Assistant Mawalla Advocate na pia ni Model Myler Nyangasa, Mwasisi na CEO wa Missie Popular Blog Mariam Ndabagenga na Fashion Stylist wa Fashionnjukii.com Rosemary Kokuhilwa.
Pichani Juu na Chini Models wa kike wakionyesha umahiri wa Catwalk wakati wa Audition kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki "ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013".
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Models wa kiume wakipita jukwaani mbele ya majaji.
Baadhi ya Models wakiwa katika tafakari ya SIJUI NITAPITA wakati wa usaili huo kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed ambao ni wauzaji wa magari aina ya Mercedes waliodhamini onyesho la 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' akielezea kuwa Mercedes Benz imedhamini Onyesho hilo kwa mara ya kwanza kwa sababu kwanza wanamkubali Ally Rehmtullah kama mmoja wa wabunifu wenye hadhi ya juu hapa nchini na kuwa wamechagua Brand ya Mercedes Benz kwa sababu ni magari yenye kiwango cha juu na Rehmtullah ana ubunifu wa hali ya juu.
Mercedes Benz imekuwa ikijihusisha na udhamini wa 'High and Fashion Show' duniani kote pia Orchestra, Baley na Sailing matukio ambayo yanaendana na hadhi ya magari ya Mercedes. Kulia ni Chief Editor wa MO BLOG Lemmy Hipolite.
Sales & Marketing Representative kutoka RAHA Preetkamal Bansal akielezea kuwa kampuni yake imekuwa na furaha kushirikiana na Ally Rehmtullah kwa kuwa ubunifu wake ni wa hali ya juu kama wao wanavyotoa huduma za Intaneti za hali ya juu na wamekuwa wakitoa huduma ya ISP (Internet Service Provider) kwa muda wa miaka 16 kwa kiwango kilekile.
RAHA wakiwa wadhamini muhimu watawezesha watu kuona Live 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013' itakayofanyika September 8 mwaka huu ambapo Watu duniani kote wataona kupitia www.ar.co.tz
Amemalizia kwa kusema "On the day the Jungle puts on its show Our Broadband let you watch it Live".
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Quality Furniture Limited Bw. Mahad A Nur akisema wameamua kujihusisha kudhamini show hii ya Ally Rehmtullah ili kutoa ufahamu kwa umma juu ya ubora wa bidhaa wanazotengeneza na siku ya Onyesho hilo watatoa Furniture zitakazotumika sehemu ya wageni maalum (VIP).

Quality Furniture Limited wanatengeneza bidhaa zenye Quality kama lilivyojina lao na kama ilivyo show ya Ally Rehmtullah lakini pia Bw. Mahad amesema wako tayari kuwadhamini wabunifu chipukizi watakaokuja na ubunifu wenye Quality.
Majaji Aysha Mbarak Meghji na Rosemary Kokuhilwa wakibadilishana mawazo baada ya kazi kubwa ya kuchagua Models watakaoshiriki 'ALLY REHMTULLAH COLLECTION 2013'.
Hawa pia nao walikuwepo.

No comments: