Saturday, July 28, 2012

Yanga Mabingwa wapya wa Cecafa Kagame Cup 2012

Mabingwa wapya wa Mashindano ya Cecafa Kagame Cup,Timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam wakishangilia ubingwa wao huo walioutwa jioni ya leo dhidi ya Azam FC ikiwa ni mara ya pili mfululizo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika fainani hiyo,Mh. Said Meck Sadick (mwenye suti katikati) akiwa pamoja na wachezaji wa Timu ya Yanga wakati akiwakabindi Kombe la ubingwa wa Cecafa Kagame Cup 2012 jioni ya leo.
Wachezaji wa Yanga wakilizungusha Kombe hilo kwa mashabiki wao waliofurika kwa wingi uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.

Mfungaji wa goli la kwanza dhidi ya Timu ya Azam,Hamis Kiiza akiwa na kombe hilo mbele ya Mashabiki wa Yanga.
Beki wa Azam FC,Aggrey Moris akitafuta namna ya kumtoka Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Kiiza katika mchezo wa Fainali ya Mashindano ya Cecafa Kagame Cup,iliyofanyika jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Yanga imeibuka bingwa kwa mara nyingine kwa ushindi wa bao 2-0.
Heka heka uwanjani.
Kipa wa Azam akiwa haamini kilichotokea.
















No comments: