Mwenyekiti wa Mtaa wa Mjini, kata ya Kishapu Mjini, Wilaya ya Kishapu, Bw. Tido Nuhu (52) akiwakaribisha Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya uliofanyika kijijini hapo.ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano kijijini hapo juzi (Jumatano, Julai 25, 2012).
Bi. Faida Faki Kombo wa Shehia ya Makombeni, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika Makombeni leo (Ijumaa, Julai 27, 2012).
Bi. Siwema Shabaan Mbato, mkazi wa kijiji cha Bwilingu, Tarafa ya Msoga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya katika mkutano uliofanyika kijini hapo leo (Ijumaa, Julai 27, 2012)
Wakazi wa kijiji cha Bwilingu, Tarafa ya Msoga, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani wakisoma kitabu kinaelezea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa lugha nyepesi. Wakazi hao walihudhuria mkutano wa kukusanya maoni yao kuhusu Katiba Mpya uliotishwa na Tume kijijini hapo leo (Ijumaa, Julai 27, 2012) - Picha kwa hisani ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba
Bi. Aziza Juma (27), mkazi wa Wilaya ya Kishapu, mkaoni Shinyanga akitoa akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano kijijini hapo jana (Alhamisi, Julai 26, 2012)
Wananchi wa Kijiji cha Maganzo, Kata ya Songwa, Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wakifuatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya jana (Alhamisi, Julai 26, 2012)
Bi. Scholastica Benard, mwenye umri wa miaka 30, mkazi wa Kata ya Minziro, Wilaya ya Misenyi, mkoani Kagera akitoa maoni yake kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilipofanya mkutano wake wilayani hapo hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba katika picha ya kumbukumbu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Michungwani iliyopo kijiji cha michungwani, Kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga mara baada ya mkutano wa kukusanya maoni kuhusu Katiba Mpya.
No comments:
Post a Comment