Thursday, July 19, 2012

SHUGHULI ZA KUTAMBULIWA MAITI ZILIZOOKOLEWA KATIKA AJALI YA MELI ZIKIENDELEA ZANZIBAR

Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana zikitambuliwa na Ndugu zao na kuruhusiwa Kuzichukuwa kwa ajili ya Kufanya taratibu za mazishi hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Learnhat Alfonso wakatikati akionekana na huzuni Baada ya kuziona Maiti zilizookolewa katika Meli iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe Zanzibar.Balozi alifika katika Viwanja vya Maisara ili kuona namna shughuli za kushughulikia maiti zinavyoendelea.
Mama alietambulika kwa Jina la Bitatu Uyelo ambae amenusurika na Kupoteza Mtoto wake wa miezi tisa katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Bahari ya Chumbe ikitokea Dare es salaam.
Waziri wa Mamboya ndani wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Emanuel Nchimbi alifikakatika Eneo lililohifadhiwa Maiti wa Ajali ya Meli ya Skagit ili kutambuliwa na Ndugu zao na Kupata maelezo kwa Daktari Kiongozi hayupo pichani Hapo katika Viwanja Vya Maisara Zanzibar.
Baadhi ya Maiti zilizookolewa kutoka katika Meli iliozama na kukosa watu wake zikipelekwa kuzikwa na Serikali katika Eneo la Kama lililotayarishwa makusudi kwa ajili hio.

2 comments:

Anonymous said...

Tuwape pole wote waliopotelewa na ndugu zao katika janga hili. Nina swali pia kwa wanablogu, hivi maiti inaokolewa au inaopolewa toka majini?.Nawasilisha.

Anonymous said...

Nimesikitishwa sana na tukio la kuzama kwa meli hapo zanzibar, cha kusikitisha ni kwamba kwanini meli zinaruhusiwa kusafiri na kuhatarisha maisha ya abiria.
Je vyombo husika kama idara ya hali ya hewa haiwezi kutia tahadhari kwamba hali ya bahari ni chafu sana na meli kuzuiwa kusafiri kwa muda huo ambapo bahari inakuwa chafu.
Watanzania lazima kubadilike na tuende na wakati, tutumie fursa ya kutumia vizuri teknologia kwa busara na faida yetu sote.
Kama idara husika ingetangaza kwamba hali ya bahari muda wa mchana kwa siku hiyo ilukuwa mbaya sana na meli kukatazwa kusafiri basi naamini wazi, tusingekuwa tuna majonzi.
Lazima tubadilike