Thursday, July 19, 2012

MATUKIO YA LEO KATIKA VIWANJA VYA MAISARA BAADA YA AJALI YA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOKEA JANA

Baadhi ya Wananchi waliozitambua maiti zao katika Viwanja vya Maisara wakisaidiwa na Askari kutokana na Huzuni kubwa waliokuwanazo.kwa kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika Foleni ili kwenda kuzitambua Maiti zao katika Viwanja vya Maisara kutokana na kuzama kwa Meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Maiti zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit iliozama zikiwa katika Eneo la Maisara kwa ajili ya kutambuliwa na Nduguzao.
Baadhi ya Wageni kutoka Nchi mbalimbali wakiwa katika Viwanja vya Maisara ili kujuwa Ndugu zao na kuangalia taratibu zinazofanyika viwanjani hapo kutokana na Kuzama kwa meli ya skagit hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamekusanyika katika Viwanja vya Maisara ili kuweza kupata taarifa ya Ndugu zao waliokuwa katika Meli ya Skagit ambayo imepata Ajali ya Kuzama katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa Vyombo mbaliombali wakiwa katika Viwanja vya Maisara ili kuweza kupata Taarifa mbalimbali za kuletwa kwa Maiti ambazo zimepatikana katika ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Wananchi mbalimbali wakizitambua Maiti zao zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Baadhi ya Maiti zilizopatikana katika Ajali ya Meli ya Skagit ilizama zikiteremshwa katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar ili kutambuliwa na Jamaa zao.
Madaktari wakiandika Orodha ya Maiti zinazoletwa hapo katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar Baada ya kupatikana kutoka katika Meli ya Skagit iliozama hapo jana katika Eneo la karibu na Kisiwa cha Chumbe Zanzibar.
Wahusika wa Matayarisho ya Mazishi ya watu waliokuwa bado hawajatambuliwa na Jamaa zao ili kuzikwa kiserikali wakiwa katika kazi ya kutayarisha Sanda hapo katika Viwanja vya Maisara Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR.

No comments: