Thursday, July 26, 2012

Mchezaji wa zamani wa Simba Issa Kihange afariki dunia

 Picha ya Marehemu Issa Kihange, baba Mzazi wa Bi Zainab Issa Kihange ambaye ni mfanyakazi wa ofisi za Bunge.  Marehemu alikuwa mchezaji mpira wa miguu mahiri aliyewahi kuichezea Timu ya Simba. Alifariki ghafla tarehe 24/7/2012 na kuzikwa nyumbani kwake Dodoma leo tarehe 26/7/2012
 Spika Makinda akiwafariji wafiwa
 Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda  (kati) akimfariji mke wa arehemu Issa na mama mzazi wa Zainab kulia. Kushoto ni Bi Zainab Issa Kihange ambaye ni mfanyakazi wa Ofisi ya Bunge.
 Viongozi wa wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge kwenye Msiba huo mapema leo
 Wafanyakazi wa Ofisi ya Bunge wakiomboleza.
 Ndugu, jamaa na majirani waliofika kwenye msiba.

     Wafanyakazi wenzake na Bi Zainab
 Mwakilishi wa Ofisi ya Bunge Ndugu Jossey Mwakasyuka akitoa salamu za rambirambi
 Ndipo ikaanza safari ya mwisho ya Issa Kihange hapa duniani
Ni vilio, ni simazi, ni majonzi, ni huzuni kubwa. Picha zote na mdau Prosper Minja wa Bunge

No comments: