Thursday, July 26, 2012

Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Morogoro

 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiweka mkuki kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa walipinga vita vya  Kagera uliojengwa katika  mzunguko wa Pota , Manispaa ya Morogoro
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiweka ngao kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa walipinga vita vya  Kagera uliojengwa katika  mzunguko wa Pota , Manispaa ya Morogoro
 Mkuu wa Shule ya Mafunzo ya Huduma na Utawala Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) Pangawe , kilichopo Mkoani Morogoro, Kanali Harrison Masebo , akipiga saluti baada ya kuweka sime na shoka kwenye mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa waliokufa wakati wa vita vya  Kagera
 Askari wa zamani aliyewahi kupigana vita kuu ya pili ya Dunia, Edward Lihamba, akisindikizwa kwenda  kuweka upinde na mishale kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wa vita vya Kagera katika mzunguko wa Posta , Mjini  Morogoro , wakati wa gwaride maalumu la kukumbuka  siku ya Mashujaa hao Julai 25,mwaka huu,
 Askari wa zamani aliyewahi kupigana vita kuu ya pili ya Dunia, Edward Lihamba, akijiandaa kuweka upinde na mishale kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wa vita vya Kagera katika mzunguko wa Posta , Mjini  Morogoro
 Heshima kwa mashujaa
 Mshikemshike wakati wa upigaji wa mizinga  mitatu ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka mashujaa.
 Wanahabari wakiwahoji wazee wawili aliopigana vita kuu ya pili ya Dunia , Edward Lihamba ( mwenye fulana ya CCM) na mwezake Salum Mlapakolo
 Ofisa na Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro wakitoa heshima kwa kipiga saliti wakati wa wimbo wa taifa
Luteni Sarah  Mwandesile akiongoza gadi ya askari wa JWTZ wakati wa gwaride la maadhimisho ya Mashujaa Julai 25, mwaka huu kuekelea mnara wa kumbukumbu ya mashujaa eneo la Posta Morogoro 
Picha zote na John Nditi wa Globu ya Jamii

No comments: