Sunday, June 10, 2012

MAJINA YA WALIOTEULIWA KUWANIA TUZO YA WANAMICHEZO BORA MWAKA 2011/MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011, ITAKAYOFANYIKA JUNI 14 MWAKA HUU


KIKAPU:
WANAWAKE
DORITHA  MBUNDA :-JKT QUEENS
EVODIA  KAZINJA:-JKT QUEENS
FARAJA MALAKI:-JESHI STARS
WANAUME
ALPHA KISUSI-Vijana 
FILBERT MWAIPUNGU:-ABC
GILBERT BATUNGI:-ABC
NETIBOLI:
LILIAN SYLIDION
 DORITHA MBUNDA
 GOFU
WANAWAKE:
Madina Iddi (Umri miaka 27)
Hawa Wanyeche (Umri miaka 26)
Ayne Magombe (Umri miaka 24)

WANAUME:
Frank Roman
Nuru Mollel
Issac Anania
GOFU WA KULIPWA:
FADHILI  SAIDI NKYA.
YASINI SALEHE
HASSANI KADIO

OLIMPIKI MAALUM
Ahmada Bakar
Amina Daud Simba-kisahani na tufe
Othman Ally Othman-mkuki, kisahani na tufe.
Cio..
PARALIMPIKI
WANAUME
ZAHARANI MWENEMTI
JOSEPH NZIKU
YOHANA MWILA
WANAWAKE
FAUDHIA CHAFUMBWE
SIWEMA KILYENYI
JANETH MADISE
NGUMI ZA RIDHAA
SULEIMAN SALUM KIDUNDA
VICTOR NJAITI
ABDALAH KASSIM
CIO…

WAOGELEAJI
(WANAWAKE)
MAGDALENA MOSHI
GOURI KOTECHA
MARIAM FOUM

WANAUME
AMMAAR GHADIYALI
OMARI ABDALLAH

JUDO...
 MBAROUK SELEMANI MBAROUK
UNDER 81KG MEN JUDO PLAYER
 MOHAMED KHAMIS JUMA
OVER 90KG MEN JUDO PLAYER
 AZZAN HUSSEIN KHAMIS
UNDER 60KG Judo player

CIO…
WAVU…

WANAWAKE
ZUHURA HASSAN-JESHI STARS
THERESIA Ojode -JESHI STARS DAR
EVERLYNE ALBERT- MAGEREZA
WANAUME
MBWANA ALLY- MZINGA CORPORATION  - MOROGORO
KEVIN PETER -MAGEREZA – DAR
FARHAN ABUBAKAR- MAFUNZO ZNZ
CIO…
NGUMI ZA KULIPWA
Benson Mwakyembe
Nasibu Ramadhan
Francis Cheka
Nassib Ramadhan
Fadhil Majia

TENISI:
WANAUME
WAZIRI SALUMU
 OMARY ABDALAH
HASSANI KASSIMU

WANAWAKE
REHEMA ATHUMANI
 MKUNDE IDDY
VIOLET PETER
Cio…

BAISKELI
Wanawake
Sophia Hussein
Sophia Anderson
WANAUME:
Richard Laizer
Hamisi Hussein

WACHEZAJI WA TANZANIA WANAOCHEZA NJE
Henry Joseph-Soka
Mbwana Samatta-Soka
Sophia Mwasikili-Soka
MCHEZAJI BORA CHIPUKIZI
Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars)
SHOMARI KAPOMBE- (soka) SIMBA
Salum Abubakari-Azam (soka)
MCHEZAJI WA NJE ANAYECHEZA TANZANIA
Haruna Niyonzima-Yanga (soka)
Kipre Tchetche-Azam (soka)
Emmanuel Okwi-Simba (soka).

SOKA (WANAWAKE)
Asha Rashid-Mburahati Queens
Mwanahamisi Omary-Mburahati Queens
Fatuma Mustapha-Sayari
Ito Mlenzi-JKT

WANAUME
John Bocco-Azam
Aggrey Morris-Azam
Juma Kaseja-Simba
RIADHA
WANAWAKE
Zakia Mrisho
Mary Naali
Jaqueline Sakila

WANAUME
Dickson Marwa
Alphonce Felix

MIKONO
WANAWAKE
Abinery Kusencha-JKT Ruvu
Kazad Mtong-Magereza Kiwira
Faraji Shaibu  Khamis-Nyuki Zbar
WANAUME:
Doris Mangara-Magereza Kiwira
Zakia Seif-Ngome Dar
Mary Kimiti-Magereza Kiwira.
Cio…
KRIKETI
WANAWAKE
MoniCa Pascal
Asha Daudi
Esther Wallace

WANAUME
Kassimu Nassoro
Benson Mwita
Riziki Kiseto

TUZO YA HESHIMA-ITATANGAZWA SIKU HIYO
NA MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA 2011
ATAPATIKANA MIONGONI MWA WASHINDI WA KILA MCHEZO.

MASOUD SANAN-
MWENYEKITI KAMATI YA TUZO
08/06/2012




Galacha kuwatuza Wanamichezo TASWA
Na Mwandishi Wetu
TOVUTI ya Kandanda.galacha.com ya jijini Dar es Salaam imejitosa kudhamini Tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2011 upande wa soka.

Wakizungumza kwenye mkutano na waandishiwa habari Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa tovuti hiyo, ambayo pia ina tovuti nyingine iitwayo kandanda.co.tz, Erick Zomboko alisema tovuti yao inahusiana na masuala ya mpira wa miguu na wameona wajiunge katika hatua ya kuendeleza michezo hapa nchini.

Alisema wanathamini tuzo hizo zinazotolewa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), hivyo pamoja na upya wao katika masuala ya tasni ya habari wameona waunganishe nguvu kusaidiana na TASWA.

Alisema katika udhamini wao watatoa tuzo maalum kwa washindi upande wa mpira wa miguu na pia watatoa fedha taslimu kwa washindi hao, lakini hawawezi kutangaza kiasi cha fedha watakachowapa washindi hadi siku hiyo.

Zomboko alitaja watakaowania tuzo hiyo kuwa ni wale waliotangazwa na Kamati ya Tuzo upande wa mpira wa miguu kwa wanaume, ambao ni Juma Kaseja (Simba), Aggrey Morris na John Bocco wote wa Azam, wakati mpira wa miguu wanawake ni Fatuma Mustapha (Sayari),  Ito Mlenzi (JKT), Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ na Asha Rashid ‘Mwalala’ wote wa timu ya Mburahati Queens.

Wachezaji wengine ambao watawania tuzo hiyo ni wale wa nje wanaocheza soka Tanzania, ambao ni Haruna Niyonzima (Yanga), Emmanuel Okwi (Simba) na Kipre Tchetche (Azam).

“Haya ni makundi matatu tofauti, ambayo yametangazwa na Kamati ya Tuzo ya TASWA, tutakachofanya sisi mshindi wa kila kundi tutampa zawadi yake siku hiyo ya sherehe, itakuwa ni tuzo pamoja na kiasi fulani cha fedha, tuzo ambayo itakuwa na jina la mhusika,” alisema na kuongeza kuwa udhamini huo ni kiasi cha sh. Milioni sita.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa TASWA inayoandaa tuzo hizo, Maulid kitenge aliishukuru tovuti hiyo na kusema licha ya kwamba wana udhamini wa Kampuni ya Bia ya Serengeti, lakini bado hautoshi, hivyo wadau mbalimbali wanakaribishwa kuwaunga mkono katika juhudi zao za kuwatuza wanamichezo.

Sherehe za kuwazawadia Wanamichezo Bora wa Tanzania zinatarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, ambapo michezo mbalimbali itazawadiwa.

Wakati huohuo, Kitenge alisema Jumatatu saa tano asubuhi TASWA wanataraji kufanya mkutano na waandishi wa habari, ambao pamoja na mambo mengine watatangaza mgeni rasmi wa sherehe hizo pamoja na burudani mbalimbali kwenye mgahawa wa City Sports Lounge.



No comments: