Monday, May 21, 2012

Ze Fulanazzzzz ndani ya Washington DC na Maryland....

 Ankal akila pozi na mdau jijini Washington DC
 Ankal na mmiliki wa kiota maarufu cha minuso cha Swahili Village, Maryland
 Dah! Hii nguna ya hapa Swahili Village balaa....
 Ankal na brother Libe ndani ya Swahili Village - Thanx Libe for the dina la mchana hapo Swahili village. You owe me one...
 Ankal na wadau wa Maryland wakiwa uwanga wa SoccerPlez Stadium 'Shamba la Bibi' uliopo  Ager Road,  Hyattsville,  Maryland kuangalia mtanange wa soka kati ya DMV United na Ureno 
 Ankal akiwa amebana njenje na wana DMV wakati wa gemu
 Ankal na bother Libe akifuatilia mtanange
 Ni mapumziko na kocha mchezaji akiwapa somo wana DMV United
 Kikosi kabambe cha DMV United
 Ankal akiangalia gemu na wadau wa DMV
 Gemu likiendelea
 Mwanalibeneke wa Swahilivilla akiwa kazini
 Ankal na Dean Nyalusi ndani ya nyumba
 Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Mh Iddy Sandaly (wa nne kulia, mbele) alikuwepo kutoa sapoti kwa timu yetu
 Ankal na wadau wakila pozi baada ya gemu
 Ankal na wadau
 Wadau wa DMV
 Ankal na wadau
 Ze Fulanazzz bin konozzzzzz....
 Bendera yetu yapepea
 Mdau anataka kupora Ze Fulanazzzzzz
 Mwanalibeneke wa Swahilivilla akimuaga Ankal akiwa na wadau na baiskeli ya kuazima
 Ankal na mdau wa toka enzi za YMCA
 Ankal na Mdau
 "Sisi sote ni ndugu wa baba mmoja...! anasema Ankal akiwa na wanalibeneke wa Vijimambo (shoto) na wa Swahilivilla
Ankal akila konozzzz na ankal.



Mchezo wa lingi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea kila wiki kwenye viwanja vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani, leo hii Mei 20, 2012 timu ya Tanzania DMV imecheza na Timu ya Portugal na kufungwa kwa taabu sana bao 2-1 katika kiwanja cha SoccerPlex Stadium uliopo Ager Road Hyattsville Maryland, wachezaji mnaombwa kufika mapema kabla mechi kuanza.

Katika mashindano hayo ya  ligi ya 2012 Diaspora World Cup, Kundi (B) Timu ya Portugal walipoteza mechi mbili ambapo  moja walifungwa bao 8-0 dhidi ya Morocco jumamosi ya Mei 5, 2012 na makapu ya magoli yalionekana tena Jumamosi ya wiki iliopita Mei 12,2012, ambapo walibamizwa na Timu ya England mabao 9-0.

Pia timu ya waTanzania DMV katika mchezo wao wa kwanza siku ya Jumapili ya April 29,2012 walifanikiwa kuwabamiza timu ya Ghana bao 3-2 kwenye ya uwanja wa SoccerPlex Stadium uliopo Ager Road Hyattsville Maryland.,vile vile mechi ya pili walitoka sare bila ya kufungana na Timu ya Ethiopian, baada  ya kusemekana  makocha wa timu hiyo kufanya ajizi ya kutochezesha baadhi ya wachezaji ambao wana matumaini makubwa ya kumili mpambano huo.
Timu ya wa Ethiopian inasemekana walimiliki mchezo huo pale walipokuwa wakibadilisha wachezaji wao kila baada ya dakika 20 wa mpambano huo na kusababisha mechi hiyo kutoa drow na Timu ya Watanzania DMV.







1 comment:

Anonymous said...

BIg Up ankal unatuletea vitu adimu
thanks