Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi kujadili ratiba ya maandalizi ya mazishi ya Mhe. Regia Mtema katika ofisi za Bunge jana. walioko kulia ni Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (Mb), Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe (Mb) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge Mhe.William Lukuvi.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda (Mb) akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi kujadili ratiba ya maandalizi ya mazishi ya Mhe. Regia Mtema katika ofisi za Bunge jana.
Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe akifafanua jambo wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichokaa jana chini ya uenyekiti wa Mhe. Spika kujadili ratiba ya maandalizi ya mazishi ya Mhe. Regia Mtema katika ofisi za Bunge. Kulia ni Mhe. Zaituni Buyogela (Mb) na Mhe. Maua Daftrari. mwenye suti kushoto ni Mhe. William Lukuvi. Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: MAANDALIZI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU
MHE. REGIA ESTELATUS MTEMA, (MB), TAREHE 17 JANUARI, 2012 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE NA MAZISHI IFAKARA, KILOMBERO, MOROGORO – TAREHE 18 JANUARI, 2012
- UTANGULIZI
Marehemu Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema alifariki kwa ajali ya gari katika eneo la Ruvu, mkoani Pwani mnamo majira ya saa 5.30 asubuhi tarehe 14 Januari, 2012. Ofisi ya Bunge baada ya kuthibitisha kifo hicho kupitia Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani na baada ya Kuwasiliana na familia, mara moja ilituma Maafisa Waandamizi kwenda katika Hospitali ya Tumbi mkoani Pwani kuuchukua Mwili wa marehemu na kuuleta Muhimbili kuhifadhiwa ikiwa ni pamoja na kufanya maandalizi ya mazishi. Baada ya maandalizi hayo na kwa ushirikiano na familia na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni yafuatayo yamekubaliwa kufanyika:-
- MWILI KUAGWA NA FAMILIA TAREHE 16 JANUARI, 2012 KATIKA KANISA KATOLIKI SEGEREA
Familia imeandaa Misa ya Marehemu katika Kanisa Katoliki Segerea siku ya Jumatatu tarehe 16 Januari, 2012 kuanzia saa 9 alasiri mpaka saa 11 jioni. Mwili wa Marehemu utaondoka Hospitali ya Muhimbili saa 7 mchana na baadae kurejeshwa tena kwa hifadhi baada ya Misa.
- MWILI KUAGWA RASMI KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE TAREHE 17 JANUARI, 2012
Ofisi ya Bunge imeandaa utaratibu kwa viongozi wa kitaifa, Waheshimiwa Wabunge, Wananchi kuuaga rasmi Mwili wa Marehemu katika viwanja vya Karimjee siku ya Jumanne tarehe 17 Januari, 2012. Shughuli hiyo inatarajiwa kuanza saa 3.00 asubuhi na kuhitimishwa saa 5.30 asubuhi (Ratiba imeambatanishwa kama kiambatisho A). Kama ratiba inavyoonesha, Mwili wa Marehemu utaondoka katika viwanja vya Karimjee saa 5.30 asubuhi mara tu baada ya kuaga katika viwanja vya Karimjee kuelekea Ifakara, Kilombero mkoani Morogoro kwa mazishi.
- RATIBA YA MAZISHI YATAKAYOFANYIKA IFAKARA
Ratiba ya tarehe 18 Januari, 2012 ambayo ndio siku ya Mazishi nyumbani kwa Marehemu Ifakara, Kilombero Mkoani Morogoro imepangwa kwa kuzingatia mila na desturi za familia. Ratiba hiyo ni kama ilivyo katika kiambatisho B. Kwa ratiba hiyo, shughuli zimepangwa kuanza saa 5 kamili asubuhi na kukamilika saa 10.30 alasiri.
- MAANDALIZI MENGINEYO
Mpaka hivi sasa familia imearifu kuwa Msiba huo umepokelewa kwa hisia kubwa katika eneo alilozaliwa Marehemu Mheshimiwa Regia Estelatus Mtema na kwamba tujiandae kwa ushiriki kwa wakazi wa Kilombero takriban 1000. Aidha, Ofisi inaendelea na Maandalizi ikiwa imejiandaa kwa ushiriki wa viongozi wa kitaifa Mkoani Morogoro.
- SHUGHULI ZA K AMATI ZA BUNGE SIKU YA JUMANNE TAREHE 17 JANUARI, 2012
Kutokana na uzito wa tukio hili, Ofisi ya Bunge inapenda kuutangazia Umma kuwa shughuli za Kamati za Bunge kwa jumanne tarehe 17 Janauari, 2012 ambazo zinafanyika katika Ofisi ya Bunge , Dar es Salaam, zitasitishwa hadi jumatano tarehe 18, Januari, 2012
Ofisi ya Bunge inaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mhe. Regia Estelatus Mtema, (MB) mahali pema peponi. Amina.
Imetolewa na,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa
DAR ES SALAAM
16 Januari, 2012
KIAMBATANISHO A
RATIBA YA KUAGA RASMI MWILI WA MAREHEMU SIKU YA JUMANNE
TAREHE 17 JANUARI, 2012 KATIKA VIWANJA VYA KARIMJEE
__________________
SN. | MUDA | TUKIO | MHUSIKA |
1. | 02:00 - 3:00 | Ndugu, Jamaa na Wananchi kuwasili | Itifaki |
2. | 03:00-03:25 | Viongozi wa Vyama vya Siasa, Waheshimiwa Wabunge, Manaibu Waziri, Mawaziri kuwasili na kuketi katika nafasi zao | Itifaki |
3. | 03:25 | Kiongozi wa Upinzani Bungeni kuwasili | Katibu wa Bunge |
4. | 03:30 | Mhe. Naibu Spika kuwasili | Katibu wa Bunge |
5. | 03:35 | Mhe. Spika kuwasili | Mhe. Naibu Spika |
6. | 03:40 | Mhe. Waziri Mkuu kuwasili | Mhe. Spika |
7. | 03:50 | Mhe. Makamu wa Rais kuwasili | Mhe. Spika/Mhe. Waziri Mkuu |
8. | 03:50 | Mwili wa Marehemu kuwasili kwa gwaride maalum la Sergeant-At-Arms | Katibu wa Bunge |
9. | 03:50 - 4:00 | Sala fupi | Kanisa Katoliki |
10. | 04:00 - 04:10 | Wasifu wa Marehemu | Katibu wa Bunge |
11, | 04:10 - 04:15 | Salamu na Rambirambi za Mhe. Spika | Mhe. Spika |
12. | 04:15 – 04:40 | Salamu na Rambirambi
| MC |
13. | 04:40 - 04:45 | Neno la Shukrani toka kwa familia | Mwakilishi wa Familia |
04:45 - 04:50 | Utaratibu wa safari | Katibu wa Bunge | |
14. | 04:50 - 05:50 | Kuaga Mwili wa Marehemu kulingana na Itifaki | MC |
15. | 05:50 | Mwili wa Marehemu kuondoka Uwanjani pamoja na Waheshimiwa Wabunge, Wanafamilia na Maafisa wanaokwenda Ifakara, Kilombero kwa Mazishi | MC |
16. | 06:00 | Viongozi wa Kitaifa kuondoka kulingana na Itifaki | MC |
KIAMBATANISHO B
RATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU REGIA ESTELATUS MTEMA, MB YATAKAYOFANYIKA IFAKARA, KILOMBERO, MOROGORO TAREHE 18 JANUARI, 2012
______________________________
SN. | MUDA | TUKIO | MHUSIKA |
1. | 04:00-05:00 | Wananchi, Familia na Viongozi wa Kitaifa kuwasili kulingana na Itifaki
|
|
2. | 05:00 - 06:00 | Chakula cha Mchana | Wote |
3. | 06:00 - 07:00 | Misa | Kanisa Katoliki, Kilombero |
4. | 07:00 - 07:10 | Wasifu wa Marehemu | Ofisi ya Bunge (Mwajiri) |
5. | 07:10 - 07:20 | Salaam na Rambirambi kutoka Uongozi wa Ofisi ya Bunge | Mhe. Spika |
6. | 07:20 - 07:30 | Salaam na Rambirambi kutoka kwenye Makundi mbalimbali ya Uwakilishi
| MC |
7. | 07:30 - 08:00 | Msafara wa Waombolezaji kuelekea Makaburini na Mwili wa Marehemu kwa Mazishi | Wote |
8. | 08:00 - 08:30 | Ibada ya Mazishi | Kanisa Katoliki, Kilombero |
9. | 08:30 -08:45 | Kuweka Mashada ya Maua kulingana na Itifaki | |
10. | 08:45 - 08:50 | Shukrani kutoka kwa familia | Mwakilishi wa Familia |
11. | 08:50 | Viongozi Kuondoka kulingana na Itifaki |
2 comments:
RIP mheshimiwa
mungu amlaze mahali pema peponi amen, na huyo mama pembeni ya Mh.Mbowe mbona anamwangalia Mbowe hivyo mama kakunja sura kama anakamuliwa jipu dah mama inaonekana we mkali
Post a Comment